ALIYEKUA
Waziri Mkuu, Edward Lowassa amempongeza Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu,
Benjamin Mkapa kwa kusimamia maamuzi yake hali iliyosaidia kuboresha
uchumi wa nchi.
Lowassa
ambaye ni mbunge wa Monduli, alisema licha ya kulaumiwa wakati wa
utawala wake, Mkapa alisimamia uamuzi wake na wananchi waliyaona maisha
bora kwa kuwa mfumuko wa bei ulikua ‘dijiti’ moja, lakini sasa umepanda
hadi asilimia 17.9.
Akizungumza
juzi kwenye kipindi cha dakika 45, kinachorushwa hewani na kituo cha
ITV, mbunge huyo alisema tatizo lililopo serikalini hivi sasa ni
viongozi kushindwa kuchukua uamuzi na kuusimamia bila kuogopa lawama
kama alivyofanya Rais Mkapa.
“Lazima
tufanye maamuzi na kuyasimamia… Rais Mkapa wakati wake alifanikiwa
kwenye hilo, aliyasimamia, watu walimlaumu wakamwita Ukapa, lakini
uchumi ulisimama na wote tulishuhudia.
“Bila
serikali kupunguza matumizi na kujikita kwenye kilimo cha mashamba
makubwa, tutaendelea kuwa maskini… jembe la mkono haliwezi kututoa. Hata
wakati wa Yesu watu walitumia wanyamakazi,” alisema Lowassa aliyetakiwa
kutoa tathimini yake kuhusu uchumi wa nchi hivi sasa.
Awali,
alikiri kukua kwa uchumi kutokana na ujenzi wa barabara za lami kwa
sehemu kubwa ya nchi, huku akisisitiza kwamba haujafika kwenye mifuko ya
wananchi kwa vile mfumuko wa bei upo juu.
Muda
mwingi wa mahojiano yake, Lowassa ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge inayoshughulikia mambo ya nje, ulinzi na usalama
aliitaka serikali kuhamasisha kilimo cha mashamba makubwa na matumizi ya
zana za kisasa za kilimo.
“Serikali
isimbane mkulima mdogo, imwache auze mazao yake popote alipo kwa
ghamara nzuri, hii itamhamasisha na kuongeza bidii kwenye uzalishaji
wake akiamua hata kuuzia Kenya,” alisema mbunge huyo.
Mafuta na Gesi
Kuhusu
kugundulika kwa rasilimali ya mafuta na gesi hapa nchini, mwenyekiti
huyo ambaye hivi karibuni aliunga mkono kauli ya serikali kuhusu mgogoro
wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi, alisema isiposimamiwa vema uwepo
wake utakuwa laana kwa Watanzania.
“Hii
ni rasilimali nzuri kwetu, tukiisimamia vema itakuwa neema na
tukiisimamia vibaya itakuwa laana… hatuna haraka ya kugawa vitalu vyote
vyenye gesi.
“Tungojee
tusiwe na haraka kama alivyofanya Mwalimu Nyerere baada ya kugundua
kwamba kuna madini aliyaacha kwanza na leo yanatusaidia, wapo
watakaoniona mjinga, lakini ‘am not a fool’ (mimi si mjinga),” alisema
Lowassa kabla ya kuhitimisha mazungumzo yake.
Kuhusu balozi zetu
Lowassa
alisema, tatizo la fedha linazikabili balozi za Tanzania nje ya nchi na
watendaji wake ambao wakati mwingine hukaa hadi miezi mitatu au sita
bila kupata mshahara.
“Nirudie
kusema ucheleweshaji wa maamuzi ni kikwazo mfano pale New York jengo la
ubalozi wetu linatakiwa kukarabatiwa, fedha inayotakiwa ni dola milioni
moja ambapo likiwa zuri tuna uwezo wa kulipangisha kila mwezi tutapata
dola 400,000, lakini hadi sasa lipo tu linazidi kuharibika.
“Pale
London, pia kuna kiwanja chetu kinavamiwa na vibaka ambao wakikaa pale
kwa wiki mbili, kuwaondoa lazima uende mahakamani, hizi zote ni mali
ambazo zinahitaji maamuzi tu zifanyiwe kazi.
“Tunao
uwezo wa kuwaambia NSSF wajenge balozi zetu huko nje tuwalipe taratibu,
lakini maombi yalipelekwa wizara ikakataa kwa kutumia sheria fulani
fulani, lakini si sahihi kutegemea fedha za bajeti kuu kwa ajili ya
ujenzi wa nyumba za serikali,” alisema.
Kuhusu afya yake
Lowassa
alianza kwa kuwalaumu waandishi wa habari wanaopotosha kuhusu afya yake
kwamba amepata kiharusi huku akikanusha kwamba alikwenda nchini
Ujerumani kwa kutizama afya yake na kufanyiwa uchunguzi wa jicho.
“Nashangazwa
na ‘speed’ ya kuandika uongo kuhusu afya za watu, siumwi na wala
sijapata kiharusi, nipo fiti kwa jambo lolote,” alisisitiza Lowassa
ambaye Machi mwaka huu safari yake ya Ujerumani ilizusha hofu juu ya
afya yake.
na tanzania daima
its normal, kitu huonekana uzuri wake baada ya kuwa mmekikosa,
ReplyDeletethe same way mtakuja kusema hivi hata akiondoka nani?
bali wanaosifiwa wakati wapo madarani hutaftiwa namna ya hizo sifa zao kufutwa kama ilivyo kwa rais mwinyi
YEAH KAKA NI KWELI
ReplyDelete