KADA
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Maliki Marupu kutoka wilayani Ulanga,
mkoani Morogoro, ametangaza nia kuwania nafasi ya uenyekiti wa CCM
taifa, inayoshikiliwa na Rais Jakaya Kikwete.
Marupu
ambaye amejitambulisha kuwa ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM Taifa,
alisema kuwa amefikia hatua hiyo ili kuleta mabadiliko ndani ya chama
hicho tawala.
Wiki
iliyopita, gazeti hili liliripoti taarifa za kuwapo kundi linalompinga
Rais Kikwete kutaka kutenganisha kofia ili asiendelee kuwa Mwenyekiti wa
CCM taifa, na kumpa nafasi ya kubaki kwenye kiti cha urais.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Marupu alisema kama
fomu za kuwania nafasi hiyo zitatolewa, ataandika historia mpya ndani ya
chama hicho.
Hata
hivyo, chini ya utaratibu wa sasa wa CCM, nafasi ya mwenyekiti taifa
haigombewi, bali jina la mgombea ambaye kwa kawaida huwa ni Rais wa
Muungano huteuliwa na Kamati Kuu (CC), kuthibitishwa na Halmashauri Kuu
(NEC) na hatimaye kupigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu.
Huku
akinukuu Katiba ya CCM, alisema ibara ya 14 kifungu kidogo cha 3,
kinampa nafasi mwanachama yeyote ndani ya chama hicho kuwania nafasi
katika ngazi yoyote.
“Unajua
lazima tuwe wazi. Kinachoogopwa hapa ni kama ikitokea mwenyekiti akawa
sio rais, iwapo patatokea kutoelewana kati yao, basi mwenyekiti wa chama
ana uwezo wa kushawishi wanachama wakamvua madaraka rais,” alisema.
Marupu alisema, utaratibu unaotumika wa kumpata mwenyekiti, umekuwa ukidumaza demokrasia ndani ya chama hicho.
Kada
huyo alisema, wapo watakaomuona msaliti ndani ya chama, lakini
amelazimika kuwania kiti hicho kuleta mabadiliko yanayoenda na wakati.
“Wajumbe
wakinipitisha, mchuano wangu na Kikwete utakuwa kama ule uliowahi
kutokea nchini Afrika Kusini kati ya aliyekuwa rais, Thabo Mbeki na rais
wa sasa Jacob Zuma aliyeibuka mshindi,” alisema.
na tanzania daima
No comments:
Post a Comment