Mtu
mmoja aitwae Msindi Kasaki anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka 68 mkazi
wa kata ya Ololangulu wilayani Uyui mkoani Tabora, anashikiliwa na jeshi
la polisi mkoani humo kwa tuhuma za kukutwa na mabomu manne nyumbani
kwake.
Kamanda
wa Polisi mkoani Tabora Anthony Rutta amesema kukamatwa kwa mtuhumiwa
huyo anaesadikiwa kuwa ni mganga wa tiba za asili kumefanikiwa baada ya
taarifa kutoka kwa msamaria mwema.
Amesema
baada ya hizo taarifa askari walikwenda kwenye eneo hilo ambapo baada
ya upekuzi na kumuhoji, Msindi alikiri kuhifadhi mabomu hayo ambayo
alikua ameyachimbia chini ya ardhi nyuma ya nyumba yake yakiwa ni mabomu
manne ya kutupa kwa mkopo ndani ya mfuko.
Kamanda
Rutta ameongeza kwamba utafiti uliofanywa na polisi inasemekana hayo
mabomu yaliagizwa nchi jirani na lilikua limeandaliwa tukio kwenda
kufanya uhalifu kwenye mnada mmoja mkoani Tabora.
No comments:
Post a Comment