
Usain
Bolt akiangalia medali yake ya dhahabu baada ya kushinda jana katika
mbio za mita 200 ikiwa ni dhahabu yake ya pili katika mashindano
yanayoendelea ya Olympiki.

Aliachukua
kamera toka kwa mpiga picha na kuanza kupiga picha kwa mashabiki na kwa
mwanariadha mwenzie Blake alieshika nafasi ya pili hiyo jana.


Blake
akitunisha misuli huku akipigwa Picha na Bolt katika moja ya vituko
walivyofanya baada ya kuweza kushinda medali hiyo jana usiku,Blake
alishika nafasi ya Pili nyuma ya Bolt.

Blake
akiendelea kuonyesha vimbwanga kwa Mpiga picha Usain Bolt hali
iliyowavutia watazamaji waliokuwa wamejaa uwanjani hapo na kutumbuizwa
kwa muda na wawili hao baada ya kushinda medali..

Furaha ya ushindi hiyo

Hivi
ndivyo alivyomaliza mbio hizo jana baada ya kuweza kumaliza kwa 19.32
katika mbio za mita 200 ambapo alishindwa kidogo tu kuifikia rekodi yake
mwenyewe ya Beijing ya 19.30

Namba 1,2,3 zilishikwa na wanariadha wote toka nchini Jamaica

Trademark kama kawaida huikosi hiyo.....

Hiyoo sasa utamshika kweli huyoo...balaaa

Yohan Blake, Usain Bolt na Warren Weir wakisherehekea ushindi wao kwa kunyakua nafasi ya l 1-2-3 kwa nchi yao Jamaica
Usain
Bolt usiku wa Alhamisi alifanikiwa kuwa mwanariadha wa kwanza katika
historia ya michezo ya Olimpiki, kuweza kuutetea ubingwa wake kikamilifu
katika mbio zote fupi, mita 100 na vile mita 200.
No comments:
Post a Comment