Fidelis
Butahe na Zaina Malongo WAZIRI wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe
amesema rada ya kuongozea ndege kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu
Julius Nyerere iliyokuwa imeharibika tangu Agosti 3 mwaka huu,
imetengenezwa na kuanza kufanya kazi juzi saa 2:45 usiku.
Agosti
17 mwaka huu, Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) ilisema rada
hiyo iliyonunuliwa na Serikali ya Tanzania kutoka Kampuni ya Silaha ya
BAE Systems ya Uingereza ilikuwa imeharibika, ikiwa ni siku moja tangu
gazeti dada la Mwananchi (The Citizen) kuripoti juu ya kuharibika kwa
rada hiyo, hali iliyoelezwa kuwa itahatarisha usafiri wa anga nchini.
Alifafanua kwamba kifaa kilichokuwa kinasumbua kimeondolewa na kuwekwa
kingine na kuongeza kuwa wameagiza vifaa vingine vya ziada.
No comments:
Post a Comment