Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, August 8, 2012

SIMBA YARUDISHA KWA JAMII - WATEMBELEA WAGONJWA NA KUGAWA VYANDARUA - MTOTO AZALIWA APEWA JINA LA KASEJA



Sisi ni watu wa kujali jamii bwana... Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nyange 'Kaburu' (katikati) akiwa pamoja na nahodha wa timu hiyo, Juma Kaseja (kulia) na beki Juma Nyosso (kushoto) wakibeba vyandarua na zawadi nyingine kwa ajili ya kugawa kwa wagonjwa wakati walipotembelea hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam leo. Picha: Sanula Athanas
Nahodha wa Simba, Juma Kaseja akiwa katika eneo la hospitali ya Mwananyamala. Picha: Sanula Athanas

Chu chu chuuuuu.... tototoooooooo
Mchezaji mpya wa Simba aliyesajiliwa katika kipindi hiki cha usajili, Salim Kinje pia alikuwepo Mwananyamala Hospital.
Lengo letu ni kusaidia jamii hivi kila mara... Kaburu (kulia) akitoa mawili matatu wakati Simba ilipotembelea wagonjwa na kutoa zawadi leo.
Mnaonaje hali ya hapa hospitali?
Juma K. Juma akitoa chandarua kwa mgonjwa
Kaburu akiongoza msafara
Hii ndio Coaster yetu lakini basi kubwa la kisasa linakuja Agosti 15
Ezekiel Kamwaga akijiandaa kumwaga vyandarua hospitalini Mwananyamala leo

Leo sio mwisho, tutakuja tena na tena... Kaburu akizungumza na akina mama hospitalini Mwananyamala


VIONGOZI, wachezaji na wazee mbalimbali wa mabingwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba wamefanya tukio la kihistoria leo baada ya kutembelea wagonjwa kwenye Hospitali ya Mwanaymala jijini Dar es Salaam na kugawa misaada mbalimbali.

Tukio hilo nadra kuonekana likifanywa na klabu za soka nchini limeelezewa na uongozi wa Simba kuwa ni sehemu ya wiki ya maadhimisho ya siku maalum ya kila mwaka ya klabu hiyo ya 'Simba Day'.

Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Geofrey Nyange 'Kaburu' ndiye aliyeongoza msafara huo huku kwa upande wa wachezaji, kipa na nahodha Juma Kaseja ni miongoni mwa nyota walioshiriki kukabidhi misaada hiyo, akiambatana na nyota wenzake kadhaa wakiwamo Juma Said Nyosso, Kigi Makassy na kiungo aliyesajiliwa msimu huu kutoka Kenya, Salim Kinje.

Akizungumza hospitalini hapo, Kaburu alisema kuwa wamewatembelea wagonjwa na kuwapa misaada kwa vile klabu yao ni sehemu ya jamii na hivyo wanapaswa kurejesha kidogo wanachokipata kwa kuwajali watu wenye mahitaji maalum.

Akaongeza kuwa mbali na kutembelea wagonjwa, pia watatembelea baadhi ya vituo vya watoto yatima na kuwapelekea misaada mbalimbali.

No comments:

Post a Comment