Bandari ya Tanga.
Boti
ndogo iitwayo Mv. Sarwak iliyokuwa ikisafiri kati ya Tanga na Zanzibar
imezama leo kati ya muda wa saa tano za asubuhi na saa saba za mchana na
mpaka sasa watu 10 wameokolewa na kukimbiziwa hopspitali visiwani humo
huku wengine wawili wakiwa hawajulikani waliko.
Taarifa
kutoka Zanzibar zimeeleza kuwa tayari msako dhidi ya watu hao wawili
unaendelea na kwamba, majeruhi wako katika eneo la Vikokotoni visiwani
humo.
Imeelezwa
kuwa raia wawili kutoka Uholanzi na mmoja wa Ufaransa ni miongoni mwa
abiria 10 walionusurika baada ya kupatiwa 'life jacket' kabla ya kuzama
kwa chombo hicho na baadaye kuokolewa.
Kwa
mujibu wa walionusurika wameeleza kwamba, boti hiyo ndogo ilizama baada
ya pampu zake zinazotumika kuondoa maji kuharibika ghafla na hivyo maji
kujaa wakati ikiendelea na safari kati ya eneo la Pangani, Tanga na
Vikokotoni, Zanzibar.
na sanga festo
na sanga festo
No comments:
Post a Comment