Askari
wa FFU wakiwa wameimarisha ulizi baada ya vurugu kuzuka katika mtaa wa
Kongo Kariakoo jijini Dar es salaam leo jioni juu kutokana na wakazi wa
mtaa huo kugombania nyumba baina ya mpangaji na mwenye nyumba,Askari
walifika eneo la tukio na kuimarisha ulinzi hata hivyo walilazimika
kutumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya watu walioko katika maeneo
hayo wakishiriki katika vurugu
Nyumba
ambayo inasadikiwa kuleta vurugu hizo ikiwa inavunjwa na vijana wa
kampuni ya Yono Actin Mart katika mtaa wa Kongo Kariakoo jijini Dar es
salaam
Wakazi wa eneo hilo wakiwa mamedhibitiwa wasiingie katika eneo la tukio
RISASI
na mabomu ya kutoa machozi leo vimerindima maeneo ya Kariakoo baada ya
mtu mmoja kuvamia nyumba kwa zaidi ya miaka 40 akidai kuwa ni yake.
Hali
hiyo imekuja baada mmiliki halali wa nyumba hiyo, Samiri Said kushinda
kesi katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala ambapo mahakama ili mtaka mtu
huyo aliyetambulika kwa jina la Shaban Hassan kuondoka katika nyumba
hiyo.
Akizungumza
na full.blogspot jijini Dar es Salaam jana kiongozi wa Kampuni ya
Udalali ya Yono, Isaac Nguku alisema walifika eneo hilo kwa amri ya
Mahakama kwa lengo la kukabidhi nyumba hiyo kwa Said.
Alisema
hata hivyo, walipofika katika eneo hilo majira ya saa 5:00 asubuhi
walikuta kundi la vijana ambao inasadikika kuwa waliandaliwa na Hassan
kwa ajili ya kukwamisha zoezi hilo.
Nguku alisema baada ya kuona hali hiyo waliamua kuomba msaada kutoka polisi ambapo walifika na kuanza kuwatawanya vijana hao.
“Vijana
hao hawakuridhika ndipo wakaanza kuturushia mawe kutoaka kona zote
walizokuwa wamejipanga kitendo hicho kilisababisha askari kufyatua
risasi za moto juu huku wakipiga mabomu ya machozi na kuwatawanya
mbali”alisema Nguku.
Baada
ya vijana hao kutawanyika mitaa minne inayozunguuka nyumba hiyo
ilifungwa, mitaa hiyo ni pamoja na Kongo, Mkunguni, Tandamti na Mchichi.
Naye
mmiliki wa nyumba hiyo, Said alisema wavamizi hao walipanga katika
nyumbani hiyo tangu mwaka 1972 ambapo baada ya hapo wakajitengezea hati
bandia kwa lengo la kumdhulumu mama yake mzazi.
Alisema
kitendo hicho kiliwafanya wafikishe kesi hiyo mahakamani ambako
waliwakilisha hati zao ambazo zimewafanya washinde kesi hiyo, mvamizi
huyo kuamriwa aondoke kitendo alichokipinga huku akikata rufaa za mara
kwa mara lakini hata hivyo akawa anashindwa mara zote.
Nyumba
hiyo inayogombewa iko mtaa wa Karikoo kitalu namba 86, hata hivyo
wakati zoezi hilo likiendelea mvamizi huyo yuko ndani kwa ajili ya
kutumikia kifungo cha siku 21.
Hadi
fullshangwe.blogspot ikiondoka katika eneo la tukio lililokuwa
limesambaa mawe yaliyokuwa yakirushwa na kikundi hicho kinachomuunga
mkono mvamizi huyo, vijana zaidi nne walikuwa wamekamatwa na polisi huku
mmoja wao akiwa ameumia usoni kutokana na purukushani na polisi.
No comments:
Post a Comment