JESHI la Polisi
nchini limeunda tume itakayochunguza kifo cha Mwandishi wa Habari wa
Kituo cha Channel Ten, Marehemu Daud Mwangosi kilichotokea mjini Iringa
wakati Jeshi la Polisi likipambana na wafuasi wa Chadema waliokuwa
katika ufunguzi wa tawi la chama hicho katika Kijiji cha Nyololo mjini
Iringa.
Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja (pichani) amesema kuwa Uchunguzi
huo utavishirikisha vyombo vya usalama kutoka Jeshi la Polisi pamoja
na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) "Jeshi la Polisi limeunda tume
itakayowahusisha Maofisa kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ
pamoja Mkurugenzi wa Makosi ya Jinai Robert Manumba, Inspekta Jenerali
wa Polisi (IGP), Said Mwema ili kubaini ukweli kuhusu kiliochosababisha
kifo cha mwandishi huyo basi tusubiri matokeo ya uchunguzi huo" alisema
Chagonja.
"Kwa sasa tayari Ispekta Generali wa Polisi (IGP), Said Mwema yupo mjini Iringa pamoja na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba pamoja na timu yake nzima kuanza rasmi kwa uchunguzi wa tukio hilo. Alisema Kamishna Chagonja
Mwili wa Daud Mwangosi baada ya kusambaratishwa na bomu. Aliyekaa jirani ni askari ambaye alijeruhiwa katika tukio hilo
Polisi wa FFU wakipiga mabomu ya machozi kutawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa katika ofisi za tawi la chama chao
Mkuu
wa Operesheni Sangara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema
Benson Kigaila, akiwa katika gari la chama hicho pamoja na mmoja wa
majeruhi wa vurugu za polisi na wafuasi wa chama hicho
RPC katika maandalizi
Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema wakipandishwa katika gari la Polisi
No comments:
Post a Comment