Singida Nao Waandamana
Askari wa usalama barabarani akiongoza maandamano ya wanahabari wa Singida walioandamana kupinga mauaji ya mwenzao
Baadhi ya waandishi wa habari mkoa Singida-SINGPRESS wakiwa ofisi za klabu wakimsikiliza Mwenyekiti waoo, Seif Takaza
Maandamano yakiendelea katika barabara mbalimbali manispaa ya Singida
Mwenyekiti wa SINGPRESS, Seif Takaza(katikati), mratibu wa klabu hiyo Evarista Lucas(kushoto) na Shabani Msangi
Wanahabari wa mkoa wa Singida wakiwa kwenye maandamano kwenye moja ya barabara za manispaa Singida kupinga mauaji ya mwandishi
Singida
Septemba 11,2012.
WANAHABARI
Mkoani Singida wameungana na wenzao nchini kwa maandamano ya kulaani na
kupinga kitendo cha jeshi la polisi kuhusika na mauaji ya mwandishi wa
kituo cha Channel Ten mkoani Iringa Daudi Mwangosi, wakati akiwa kazini.
Kupitia
umoja wa klabu yao ya habari mkoa Singida(SINGPRESS), maandamano hayo
yakisindikizwa na askari polisi yalianzia eneo la Benki ya NBC na
kuendelea barabara ya Kawawa hadi kituo cha mafuta Esso.
Baadaye
yaliingia barabara ya Soko kuu, msikitini, Mghandi, Ipembe, Karume,
Kinyeto na kumalizikia kwenye ofisi ya klabu, kabla ya kupokelewa na
Mwenyekiti wa SINGPRESS, Seif Takaza.
Akizungumza
na waandishi 19 wa mkoa Singida walioshiriki maandamano hayo, Takaza
alisema kitendo cha polisi kuhusika na mauaji hayo kimedhalilisha chombo
hicho, pia ni ukiukwaji wa haki za binadamu, kulingana na mafunzo yao
ya kijeshi.
“Mauaji
ya mwangosi ni ya makusudi, hasa ikizingatiwa alikuwa chini ya mikono
ya polisi, lakini mwisho wa siku akafia mikononi mwao….jambo hili lazima
lipingwe kwa nguvu zote na watetesi wa haki za binadamu,”alisema.
Alisema
mauaji hayo ni ya uonevu, kikatili na yanalifedhehesha taifa ambalo
tangu lipate uhuru mwaka 1961 limejipatia sifa kubwa ya kudumu katika
hali ya amani na utulivu kiasi cha kuitwa jina la kisiwa cha amani.
Aidha
wanahabari hao wameomba kudumishwa kwa mahusiano ya jeshi la polisi na
waandishi wa wa habari ili kuondoa uwezekano wa kutokea mauaji mengine
kama hayo.
Hata
hivyo wananchi wengi, waliyaunga mkono maandamano hayo na kuwakipunga
mikono waandishi huku wakitamka neno la ‘Poleni’, kila ambako wanahabari
walipita katika barabara mbalimbali za mjini Singida.
Na Elisante John
No comments:
Post a Comment