Mabingwa wa Kombe la Vilabu Bingwa ukanda wa Afrika Mashariki na
kati, timu ya Young Africans imnefanya ziara ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza bia TBL kilichopo eneo la mchikichini Ilala.
Young Africans imefanya ziara hiyo ikiwa ni taratibu zilizowekwa na
kampuni ya TBL kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro ambao ndio
wadhamini wakuu wa timu ya Yanga.
Ziara hiyo ilianzia kwa kutembelea sehemu ya uchambuaji wa vimea,
kisha kupita sehemu ya kuanda na kuchemsha vimea, ambapo
walipata
maelezo mazuri kutoka kwa Sawe ambapo wachezaji na viongozi walionekana kuelewa zaidi maelezo yake.
Sawe aliwalezea taratibu za kuandaa bia katika kiwanda hicho,
ambapo alisema kiwanda hicho kinatengeneza bia aina 14 ambapo
kiwanda cha Dar es salaam, ndio kinaongoza kwa uzalishaji,
kiifuatiwa na Mwanza, Arusha na Mbeya.
Kocha Tom Saintfiet alisema amefurahi sana kupata nafasi hiyo
pamoja na wachezaji wake kutembelea kiwanda cha bia, ambapo
alisema anashukuru kampuni ya TBL kupitia bia ya kilimanjaro
kuwa wadhamini wa mabingwa wa soka afrika mashariki na kati.
Wachezaji pia walipita sehemu ya uchachushaji wa togwa, kabla ya
kupita sehemu ya kuchujia bia na kisha kuendelea na sehemu ya
upakiaji bia kwenye chupa, ufungwaji wa vizibo kwenye chupa na
kisha sehemu ya kupakia kwenye makreti na kufungwa kweye
maboksi kwa bia za makopo.
Utembeleaji huo wa kiwanda ulitumia masaa zaidi ya mawili na
baada ya hapo, TBL iliandaa vitafunwa na vinywaji kwa ajili ya
wachazaji na Viongozi wa Yanga, huku wafanyakazi wa TBL
wakijumuika pia katika hafla hiyo.
Akiongea kwa niaba ya uongozi, Afisa Habari wa Yanga Louis
Sendeu alisema tunashukuru TBL kwa kutupa mwaliko wa kuja
kujionea jinsi bia inavyoandalia mpaka kufikia hatua ya mwisho
ya kutumiwa na mteja, kwa kweli ni faraja sana na kukupitia
wadhamini wetu bia ya Kilimanjaro, tunasema ahsanteni sana
na sisi tunaahidi hatutawaangusha katika kuitangaza kilimanajaro
kwa kufanya vizuri katika michezo yetu ya ligi kuu Tanznaia
itakayoanza wiki ijayo alisema "Sendeu"
Kocha Tom Saintfiet alisema kwa kweli ziara imekwua nzuri,
mimi nimefurahi kutemmbelea kiwanda cha wadhamini wetu na
wachezaji wangu kwa ujumla na benchi la ufundi tumefurahi,
hatuna cha kusema sana zaidi ya kuwaahidi kuendelea kuitangaza
bia ya kilimanajaro kimataifa.
Meneja wa bia ya kilimanjaro Geroge Kavishe aliishukuru Yanga kwa
kuja kutembelea kiwanda na pia kwa kuitanagza bia ya kilimanajro nje
ya mipaka ya Tanzania, ambapo katika ziara ya maandalizi ya ligi
nchini Rwanda kupitia Yanga bia ya kilimanjaro imepata wateja
wengi na wanfaikiria hivi karibuni kuanza kupeleka kinywaji hicho huko.
Timu ya Yanga inatarajiwa kusafiri kuelekea Jinjini Mbeya katikati mwa
wiki ijayo, kwa ajili ya mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu Tanzania bara ,
ambapo katika mchezo wa ufunguzi itacheza na wenyeji timu ya
Tanzania Prisons tarehe 15 septemba 2012 katika Uwanja wa Sokoine.
No comments:
Post a Comment