Mpishi
maarufu Duniani kutoka nchini India Sanjeev Kapoor (kulia) akiongea na
waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam jinsi
vyakula vya asili vinavyoweza kuwavutia watalii kwenda kutembelea nchi
mbalimbali na hivyo kukuza utalii wa nchi husika huku Mkurugenzi
Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Nchini Dkt. Aloyce Nzuki akimsikilia kwa
makini. Mpishi Kapoor amekuja nchini kwa ajili ya kuandaa vipindi vya
runinga ambavyo vitahusu mapishi ya vyakula vya asili ili kutangaza
utalii wa kiutamaduni nchini India.
Mpishi
maarufu Duniani kutoka nchini India Sanjeev Kapoor (kulia) akimkabidhi
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Nchini Dkt. Aloyce Nzuki leo
jijini Dar es Salaam kitabu kinachoonyesha aina mbalimbali za mapishi
alizoziandaa katika kipindi cha mapishi kijulikanacho kama Khana Khazana
kinachorushwa na Televisheni ya Taifa ya India. Mpishi Kapoor atakuwepo
nchini kwa muda wa wiki mbili kwa ajili ya kuandaa vipindi vya runinga
ambavyo vitahusu mapishi ya vyakula vya asili ili kutangaza utalii wa
kiutamaduni nchini India.
Mkurugenzi
Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Nchini Dkt. Aloyce Nzuki akiwaonyesha
waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kitabu
alichopewa na mpishi maarufu Duniani kutoka nchini India Sanjeev Kapoor
kinachoonyesha aina mbalimbali za mapishi alizoziandaa katika kipindi
cha mapishi kijulikanacho kama Khana Khazana kinachorushwa na
Televisheni ya Taifa ya India. Mpishi Kapoor atakuwepo nchini kwa muda
wa wiki mbili kwa ajili ya kuandaa vipindi vya runinga ambavyo vitahusu
mapishi ya vyakula vya asili ili kutangaza utalii wa kiutamaduni nchini
India.
Baadhi
wa wageni waalikwa na mwaandishi wa habari wakimsiliza Mpishi maarufu
Duniani kutoka nchini India Sanjeev Kapoor (hayupo pichani) akielezea
umuhimu wa vyakula vya asili katika sekta ya utalii wa nchi Mpishi
Kapoor atakuwepo nchini kwa muda wa wiki mbili kwa ajili ya kuandaa
vipindi vya runinga ambavyo vitahusu mapishi ya vyakula vya asili ili
kutangaza utalii wa kiutamaduni nchini India.
Mpishi
maarufu Duniani kutoka nchini India Sanjeev Kapoor (kulia) akisaini
kitabu chake kinachoonyesha aina mbalimbali za mapishi alizoziandaa
katika kipindi cha mapishi kijulikanacho kama Khana Khazana
kinachorushwa na Televisheni ya Taifa ya India huku Mkurugenzi
Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Nchini Dkt. Aloyce Nzuki akimuangalia.
Mpishi Kapoor atakuwepo nchini kwa muda wa wiki mbili kwa ajili ya
kuandaa vipindi vya runinga ambavyo vitahusu mapishi ya vyakula vya
asili ili kutangaza utalii wa kiutamaduni nchini India.
Mkurugenzi
Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Nchini Dkt. Aloyce Nzuki (wa pili
kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na mpishi maarufu Duniani kutoka
nchini India Sanjeev Kapoor (wa pili kulia) mara baada ya kumalizika kwa
mkutano baina yao na waandishi wa habari uliohusu umuhimu wa vyakula
vya asili katika sekta ya utalii uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kulia ni Naibu Meneja Mkuu wa Hoteli ya Serena Daniel Sambai na kushoto
ni Mkurungezi wa Performance Ltd. Tanzania Runjiv Kapur.
Picha na Anna Nkinda – Maelezo
No comments:
Post a Comment