Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwanadamizi wa Jeshi la Polisi Bw. Zelothe Stephen.
Mtu
mmoja aliyefahamika kwa jina la Simon Mdugu mwenye umri wa miaka (70)
Mgogo, mkulima na mkazi wa Kisima cha Ndege Mundemu katika wilaya ya
Bahi amefariki Dunia baada ya kujeruhiwa na Ndoo Kichwani na katika Taya
na mteja wake aliyekuwa akichota maji katika kisima chake.
Akizungumzia
tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Zelothe Stephen
alisema tukio hilo lililipotiwa Polisi mnamo tarehe Tarehe 07/ 10/2012
majira ya kumi na mbili jioni (18:00 hrs) katika kituo cha Polisi
Wilaya ya Bahi.
Bw.
Zelothe alimtaja mteja huyo ambaye ni mtuhumiwa katika tukio hilo kuwa
ni Bi MAGRETH d/o JOSEPH, mwenywe umri wa Miaka (44) Mgogo, Mkulima
ambaye pia ni mkazi wa Kisima cha Ndege.
Kamanda
Zelothe Stephen alisema chanzo cha tukio hilo ni Ugomvi ulitokea siku
ya Jumamosi Tarehe 06/10/2012 Majira ya saa nne asubuhi ambapo Marehemu
alikuwa akimdai Bi MAGRETH d/o JOSEPH amlipe pesa Shilingi mia mbili
(Tsh 200/=) baada ya kuchota maji katika Kisima chake.
“Bw.
Simon Mdugu ambaye ni marehemu alimtaka Bi Magreth Joseph aliyekuwa
amejitwisha ndoo kichwani kumlipa pesa yake, mwanamke huyo alikataa na
mara ugomvi ukatokea ndipo akampiga na ndoo hiyo na kumjeruhi Kichwani
na katika Taya lake.” Alieleza Bw. Zelothe
Mkuu
huyo wa Polisi Mkoa wa Dodoma alisema baada ya mzee huyo kujeruhiwa
alikwenda kupata matibabu katika kituo cha afya cha Mdemu ambapo
alitibiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani, lakini Mnamo Tarehe 07/ 10/2012
majira ya 18:00 kamili jioni alifariki dunia
Kamanda
Zelothe Stephen alisema mtuhumiwa amekamatwa na anashikiliwa na Jeshi
la Polisi kwa mahojiano zaidi na atafikishwa mahakamani mara moja kujibu
tuhuma zinazomkabili.
Wakati
huo huo Gari namba T.624 BAD TOYOTA CRESTA lililokuwa likiendeshwa na
Jasiri Maligo, Miaka (44), Mbena, mkazi wa Ipagara lilimgonga mtembea
kwa miguu ambaye hakufahamika jina, mwanaume, umri kati ya miaka 35-40
na kumsababishia kifo.
Kamanda
Zelothe alisema tukio hilo lilitokea tarehe 07/10/2012 majira ya saa
tatu usiku, katika eneo la Chaduru kata ya Makole tarafa ya Mjini katika
Manispaa ya Dodoma kwenye barabara kuu ya DODOMA/MOROGORO.
Akizungmzia
Chanzo cha Ajali hiyo, alisema kuwa ni uzembe wa Dereva, aidha alisema
Dereva wa gari hiyo amekamatwa na atapelekwa mahakamani kwa mujibu wa
sheria.
No comments:
Post a Comment