Chama
cha Wananchi CUF kinasikitishwa na matukio ambayo hayakutarajiwa
kutokea hapa Zanzibar yaliyoanza kujitokeza tarehe 17/10/2012 ambayo
yamesababisha vurugu kubwa katika Manispaa ya Zanzibar na vitongoji
vyake.
Matukio hayo yamesababisha uharibifu mkubwa wa mali za Umma, wananchi mmoja mmoja na hata vyama vya siasa.
Miongoni
mwa vitendo hivyo ni ku... vunjwa Maduka, vyombo vya usafiri, kukatwa
miti ovyo na nguzo za umeme, pamoja na kuchomwa moto maskani za CCM.
Matukio mengine ya kusikitisha na kuhuzunisha kufuatia vurugu hizo ni
kuwepo taarifa za kuuwawa kwa Askari Polisi.
Kutokana
na vitendo hivyo, Chama Cha wananchi CUF kinaalaani kwa nguvu zote
matukio hayo ambayo yamepelekea uvunjifu wa mkubwa wa amani ya nchi, na
kusababisha hofu kubwa kwa raia pamoja na wageni wanaotembelea Zanzibar.
Sambamba
na vurugu hizo, Chama Cha Wananchi CUF kimepokea kwa mshtuko mkubwa
taarifa ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliyotolewa na Waziri wa Nchi
Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mhe. Mohammed Aboud Mohammed iliyoeleza
juu ya kutoweka kwa Sheikh Farid Hadi Ahmed katika mazingira ya
kutatanisha.
Katika
Taarifa hiyo, Serikali imethibitisha kuwa vyombo vyake vyote vya ulinzi
havijamkamata Sheikh Farid, jambo ambalo limezidisha hofu na wasi wasi
kwa wananchi juu ya mahali alipo na hali yake kiongozi huyo wa Jumuiya
ya Maimamu Zanzibar.
Chama
cha Wananchi CUF kinaiomba Serikali kuendeleza juhudi zote za
kuhakikisha taarifa za ukweli na za uhakika zinapatikana juu ya kadhia
ya kutoweka kwa Sheikh huyo kwani Sheikh Farid ni raia wa nchi hii, na
Serikali hii ni kwajili ya wananchi wote, ili kuondoa hofu na wasi wasi
ambao umesababisha baadhi ya wananchi kujengwa na dhana mbaya.
Aidha,
Chama cha wananchi CUF kinawataka wanachama wake, wapenzi na wananchi
wote kwa ujumla kutojiingiza na kutofanya vitendo vyovyote vinavyoweza
kupelekea uvunjifu wa amani ya nchi yetu.
Sote
kwa pamoja tukatae kabisa kujihusisha na vitendo vya kuleta vurugu kwa
vitendo na kauli zitakazopelekea kuiondolea sifa njema nchi hii ya
Zanzibar ambayo imejijengea duniani kote
Haki sawa kwa Wote
………………………..
Salim Biman
Kaimu Naibu katibu Mkuu Zanzibar
No comments:
Post a Comment