Shirikisho
la Ngumi la Kimataifa (IBF) katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati,
Ghuba ya Uarabu na Uajemi linawahamasisha Watanzania wajitokeze kwa
wingi kwenda kumshangilia Francis Cheka katika mpambano wake na Benjamin
Simon wa Ujerumani.
Mpambamo
huo ambao utafanyika tarehe 18 November 2012 katika ukumbi wa Universal
jijini Berlin nchini Ujerumani utawakutanisha miamba miwili
iliyosheheni kila aina ya ujuzi wa kupigana.
Watanzania wawe na tabia ya kuwaenzi wenzao wanapowakilisha taifa hili kama wenzetu wanchi nyingine kama Kenya na Uganda wanavyofanya.
Mbali
na watanzania watakaokwenda wakifuatana na Francis Cheka tokea
nyumbani, pia watanzania wanaoishi nchini Ujerumani na nchi nyingine za
Ulaya kama Uingereza, nchi za Skandinavia, Ufaransa, Uholanzi, Hungary
na nyingine wanaombwa kujitokeza kwa wingi ili waweze kumshangilia
Mtanzania mwezao aweze kupeperusha bendera ya nchi yetu vizuri.
Tayari
mtangazaji maarufu wa ITV na Radio One “Maulid Baraka wa Kitenge”
pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Jambo Concept inayomiliki magazeti ya
Jambo Leo, City Sports Lounge, Jambo Magazine Brand Tanzania bwana Juma
Abbas Pinto aliye pia mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT)
wameshaonyesha nia ya kwenda Ujerumani kulitangaza pambano hilo kwenye
vyombo vyao vya habari pamoja na kumshangilia Francis Cheka.
Bodi
ya Utalii Tanzania (TTB) inahamasishwa pia itumie nafasi hii kuitangaza
nchi yetu huko Ulaya kama zinavyofanya bodi nyingine kama za Kenya,
Botswana, Uganda, Oman na nyinginezo zinazotumia wanamichezo wake
kutangaza vivutio vya kitalii nchini mwao.
“Tunaishauri
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) izitumie nafasi ambazo watanzania
wanawakilisha nchi ili kutangaza vivutio vyake vya katalii”.
No comments:
Post a Comment