Mwenyekiti
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (kulia) akionesha
nakala ya gazeti la Jambo Leo la tarehe 20.Septemba, 2012
linalowaonyesha wafungwa na mahabusu wa gereza la Wilaya ya Mbinga,
mkoani Ruvuma wakitoa maoni yao kuhusu Katiba Mpya wakati wa Mkutano
wake na waandishi wa vyombo vya habari uliofanyika leo jumanne tarehe
9.Oktoba, 2012 katika Ofisi za Makao Makuu ya Tume hiyo Jijini Dar es
Salaam. Jaji Warioba alikuwa akitoa ufafanuzi kuhusu ushiriki wa makundi
maalum ikiwemo wafungwa na mahabusu kuhusu Katiba Mpya Kushoto ni
Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mkuu Augustino Ramadhani.
Mwenyekiti
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (katikati)
akizungumza na waaandishi wa habari leo jumanne tarehe 9. Oktoba, 2012
(hawapo pichani) kuhusu kumalizika kwa awamu ya pili ya kazi ya
ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya na kuanza kwa awamu
mpya ya tatu iliyoanza juzi jumatatu tarehe 8.Oktoba, 2012 katika mikoa 9
nchini. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti Jaji mkuu mstaafu Augustino
Ramadhani.
No comments:
Post a Comment