Akiongea na mtandao wa klabu www.youngafricans.co.tz, Daktari wa timu ya Young Africans Dokta Suphian Juma, amesema Yondani alipata mshtuko katika mfupa wake mkubwa, baada ya kuchezewa vibaya na kiungo wa timu ya Simba Haruna Moshi 'Boban'.
Dr Suphian anatoa wasi wasi wapenzi na washabiki wa Young Africans, kwamba Yondani anaendelea vzuri na anatazamiwa kurudi dimbani baada ya wiki mbili. 'Unajua Yondani baada ya kukanygwa na Boban alipata mshituko katika mfupa wake mkubwa mguuni, hivyo anapata matibabu ya kumrejesha katika hali yake ya kawaida.
Katika hali ya kushangaza mwamuzi wa mchezo huo wa watani wa jadi, Mathew Akrama alishindwa kumonyesha kadi nyekundu Boban kwa mchezo mbaya uliopelekea Yondani kutolewa nje na kushidwa kuendelea na mchezo.
Mechi hiyo ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyowakutanisha watani wa jadi wakongwe Afrika Mashariki iliishia kwa sare ya mabao 1-1, mabao yaliyofungwa na Amri Kiemba Simba dakika ya 4 na Said Bahanunzi aliyesawazisha kwa upande wa Young Africans dakika ya 67.
Young Africans leo imeendelea na mazoezi katik uwanja wa shule ya sekondari ya Loyola kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya timu ya Kagera Sugar, mchezo utakaofanyika siku ya jumapili katika uwanja wa kaitaba mjini Bukoba.
No comments:
Post a Comment