WAKATI
ikidaiwa kuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya Matonya, alifungiwa
ndani kimapenzi na mmoja ya wasanii wa bongo movie na kulizwa shilingi
za kitanzania milioni 6, sasa ameamua kuweka wazi kuwa wanawake wa
tasnia hiyo ni michosho kwani wanapemnda hela na wanaleta maigizo hadi
kwenye mapenzi.
Alipotafutwa Tonya Boy na kuzungumza juu ya ishu hiyo kuwa
kulikoni hadi alilizwa kiasi hicho cha pesa, ndipo alipodai kuwa kuna
mmoja wa mademu wazuri wanaovuma kwenye tasnia bongo movie ndiye
aliyefanya mchezo huo mchafu kwani alijifanya anampenda sana kumbe
alikuwa anamuigizia na alikuwa na ishu yake.
Alidai kuwa baada ya tukio hilo kutokeo demu huyo hakumuona tena na
alikuja kusikia yupo mkoani kitu ambacho kilimfanya aishiwe nguvu kwani
hakuamini kilichotokea na hapo ndipo alipoamini kuwa mademu wa tasnia
hiyo ni wapigaji na ukiwaonesha kwako utajuta.
“Bongo movie hakuna demu yani hata bure siwataki tena yani wanaleta
maigizo hadi kwenye mapenzi dah kweli hii tasnia ina laana na inahitaji
kuombewa kwani wasanii wake wanatamaa ya hela na wanamapepo ya ngono
yani wakimuona mwanaume ana hela basi mate yanawatoka, hata wa bure
siwataki tena,” alidai.
Hata hivyo alipoulizwa jina la msanii huyo wa filamu alishindwa kumtaja
kwa madai kuwa hata kama aliiba kiasi hicho cha pesa lakini kwa upande
wake hana bifu naye ingawa hatamani hata kumuona.
No comments:
Post a Comment