Katibu wa
Jumuiya na Taasisi za Kiislam,Sheikh Issa Ponda, na watu wengine 50
wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam
kujibu mashtaka mbalimbali
Karandiga lililowabeba Sheikh Issa Ponda na wenzake
Wanahabari wakiwa kazini
Wanahabari wakirekodi kuwasili kwa Sheik Issa Ponda Mahakamani Kisutu leo
Mmoja wa washtakiwa akitelemshwa kutoka kwenye karandinga
Picha Kwa Hisani ya Michuzi Blog
Shitaka jingine wanadaiwa wote kwa pamoja kuingia kwa nguvu kutaka kufanya makosa, huko huko Chang’ombe kwa jinai na bila sababu za msingi walivamia Ardhi katika kiwanja kinachomilikiwa na kampuni ya Agritanza kwa nia ya kujimilikisha isivyo halali
Pamoja na jitihada za wakili wao Juma Nasoro kuwaombea dhamana wateja wake lakini jitahada hizo ziligonga mwamba.
Picha Kwa Hisani ya Michuzi Blog
Katibu wa baraza la Waislam Tanzania Shekhe
Issa Ponda amepandishwa kizimbani leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu jijini Dar es salaam na kusomewa mashitaka matano.
Alifikishwa mahakamani hapo na kupoandishwa kizimbani na watu
wengine 49 akiwemo bibi wa miaka 100 kwa msafara wa magari ya polisi na ving’ora likiwemo gari la maji ya machozi kwa kasi ya ajabu na kushushwa haraka. Hata hivyo baada ya kukana mashitaka yao walirudishwa rumande baada ya kukosa dhamana.

Ponda,
aliyewasili peke yake, alipelekwa moja kwa moja katika chumba cha
mahakama na kuunganishwa na washitakiwa wenzake. Wote walisomewa
mashitaka hayo mbele ya hakimu Stewart Sanga na wakili wa serikali
Jumanne Kweka.
Wote
kwa pamoja walidaiwa kula njama, na katika maelezo ya kosa walidaiwa
Oktoba 12, mwaka huu katika eneo la Chang’ombe Markasi katika Wilaya ya
Temeke jjijni Dar es Salaam walikula njama ya kutenda kosa.
Shitaka jingine wanadaiwa wote kwa pamoja kuingia kwa nguvu kutaka kufanya makosa, huko huko Chang’ombe kwa jinai na bila sababu za msingi walivamia Ardhi katika kiwanja kinachomilikiwa na kampuni ya Agritanza kwa nia ya kujimilikisha isivyo halali
Shitaka
la tatu walidaiwa kujimilikisha kwa nguvu, maelezo ya kosa walidaiwa
wote kwa pamoja walivamia kiwanja hicho pasipo kuwa na uhalali na katika
hali ya uvunjifu wa amani, walijimilikisha mali hiyo ambayo ni mali
halali ya kampuni ya Agritanza
Aidha
katika shitaka la nne ambalo ni la wizi kati ya Oktoba 12 na 16 mwaka
huu, washitakiwa waliiba vifaa vya ujenzi walivyovikuta katika kiwanja
hicho vyenye thamani ya shilingi 59,650,000 ambavyo ni kokoto, nondo na
saruji mali ya kampuni ya Agritanza.
Shekhe
Ponda peke yake ameshtakiwa kuchochea kwa nia ya kuhamasisha utendaji
kosa katika maeneo tofauti kati ya Oktoba 12 na 16 mwaka huu, kama
katibu wa baraza la Waislam Tanzania, huko Temeke eneo la Chang’ombe,
jijini Dar es salaam.
Washtakiwa
wote walikana mashtaka hata hivyo walirudi rumande kwa sababu hakimu
aliyepangiwa kusikiliza kesi hiyo hakuwepo na hivyo kusomwa mbele ya
hakimu Sanga ambaye alisema hana mamlaka.
Mkurugenzi
wa mashitaka nchini (DPP) amewasilisha hati ya kuzuia dhamana ya Shekhe
Ponda kwa kile alichotaja kuwa ni kwa usalama wa Ponda na pia kwa
maslahi ya Jamhuri. Kesi hiyo itatajwa Novemba mosi mwaka huu na kwamba
upelelezi haujaamilika.
Pamoja na jitihada za wakili wao Juma Nasoro kuwaombea dhamana wateja wake lakini jitahada hizo ziligonga mwamba.
Msafara
wa zaidi ya magari kumi uliondoka na washitakiwa hao huku likiwemo gari
lile la maji ya machozi maaskari wa barabarani, askari magereza na
fidifosi huku Ponda akiwekwa katika gari la vioo vya giza kama
alivyoletwa.
No comments:
Post a Comment