DAKIKA 90 |
Bahanuzi anafunga penalti |
Refa Mathwe Akrama aliyeshika mpira na wasaidizi wake baada ya mechi |
Ngassa akiomba dua |
Akrama akitoa kadi nyekundu |
Bahanuzi akishangilia baada ya kufunga lla kusawazisha |
Bahanuzi akipongezwa |
Kaseja akiokoa moja ya hatari |
Berko |
Boban naAkuffo wakimpongeza Kiemba |
11 wa Yanga walioanza |
11 wa Simba walioanza |
Na Mahmoud Zubeiry
YANGA imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na wapinzani wao
wa jadi, Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uliopigwa
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kuanzia saa 1:02 usiku.
Yanga ambao walimaliza mechi hiyo wakiwa pungufu baada ya
Simon Msuva kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 77 kwa kumrudishia rafu Juma
Nyosso, ndio waliohaha kusawazisha bao, baada ya kutanguliwa kwa bao la mapema
la kiungo Amri Kiemba.
Hadi mapumziko Simba walikuwa tayari mbele kwa bao 1-0,
lililotiwa kimiani na kiungo Amri Kiemba dakika ya pili.
Simba walicheza vizuri kipindi chote cha kwanza wakigongeana
pasi za uhakika na kuwazidi kasi uwanjani wapinzani wao, wakati Yanga pamoja na
kuzinduka baada ya kufungwa bao, lakini makosa yalikuwa mengi.
Pasi zao zilikuwa nyingi hazifiki, walikuwa wanapokonyeka
mipira kirahisi, wanazidiwa nguvu na wapinzani wao katika kugombea mipira na
hata mashambulizi yao hayakuwa ya mpangilio, zaidi ya kuonekana kubahatisha zaidi.
Katika kubahatisha huko, Mbuyu Twite alifumua shuti zuri
dakika ya 38 kutoka wingi ya kulia, ambalo lilitoka nje sentimita chache.
Kabla hata ya dakika 45 za kipindi cha kwanza kumalizika,
kocha Mholanzi Ernie Brandts alimtoa Hamisi Kiiza na kumuingiza Frank Domayo
ili kuimarisha safu ya kiungo, ambayo ilionekana kuzidiwa na Simba inayofundishwa
na Mserbia, Milovan Cirkovick.
Kipindi cha pili, Yanga walianza na mabadiliko, kocha Ernie
Brandts akimtoa kiungo Nizar Khalfan na kumuingiza mshambuliaji Didier
Kavumbangu, ambaye alikwenda kuongeza nguvu ya safu ya ushambuliaji ya timu
hiyo.
Angalau, kipindi cha pili Yanga walionekana kucheza vizuri na
kupeleka mashambulizi yenye uhai langoni mwa Simba, ingawa safu imara ya ulinzi
ya Wekundu wa Msimbazi ilikuwa kikwazo.
Katika dakika ya 63, beki Paul Ngalema aliunawa mpira katika
harakati za kuokoa na refa Mathew Akrama akaamuru penalti, ambayo ilikwamisha
kimiani kiufundi na Said Bahanuzi ‘Spider Man’.
Katika dakika ya 77 Mathew Amkrama alimtoa nje kwa kadi
nyekundu ya moja kwa moja Simon Msuva, baada ya kumkita Juma Nyosso,
aliyemkanyaga ‘kwa bahati mbaya’. Msuva alichezewa rafu na Nyosso na tayari
refa alikwishapuliza filimbi na kumpa kadi ya njano beki huyo wa Simba, lakini
kiungo huyo wa Yanga akaponzwa na hasira za kitoto.
Pamoja na Yanga kubaki pungufu, waliendelea kucheza vema na
mashambulizi yalikuwa ya pande zote mbili. Refa Akrama alishindwa kuumudu
mchezo na maamuzi yake mengi yalikuwa chungu kwa Yanga, mfano Haruna Moshi ‘Boban’
alipomchezea rafu mbaya beki Kevin Yondan hadi akashindwa kuendelea na mchezo,
na nafasi yake ikachukuliwa na Juma Abdul alimpoza kwa kadi ya njano.
Hakumchukulia hatua yoyote kipa Juma Kaseja aliyeonekana
kupoteza muda tangu mwanzo, na alimpa onyo tu zaidi ya mara tatu.
Alipingia Abdul alikwenda kucheza beki ya kulia na Mbuyu
Twite akahamia katikati kucheza na Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Baada ya mchezo huo, kocha wa Simba, Milovan alisema kwamba
ulikuwa mchezo mzuri na Yanga walicheza vizuri, lakini timu yake ilicheza vizuri
na anajivunia. Alisema Yanga imeimarika tofauti na ilivyokuwa awali na kwamba
hizo ni dalili Ligi Kuu msimu huu itakuwa ngumu.
Kwa upande wake, kocha wa Yanga, mwanzoni hawakucheza vizuri,
lakini baadaye walitulia na kucheza vizuri. “Hii ni mechi ya kweli ya upinzani,
unaweza kuona rafu na kadi nyingi,”alisema Brandts.
Kwa matokeo hayo, Simba imefikisha pointi 13, ndani ya mechi
tano na kuendelea kuongoza Ligi Kuu, wakati Yanga imefikisha pointi nane na
kubaki nafasi ya tano, kwani Coastal Union imetoa sare ya 2-2 na JKT Oljoro
mjini Arusha na kufikisha pointi tisa.
SIMBA: Juma Kaseja, Nassor Chollo, Paul Ngalema, Juma Nyosso,
Shomary Kapombe, Jonas Mkude/Haruna Moshi, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Felix
Sunzu, Edward Christopher/Daniel Akuffo na Mrisho Ngassa.
YANGA: Yaw Berko, Mbuyu Twite, Stefano Mwasyika, Nadir
Cannavaro, Kevin Yondan/Juma Abdul, Athumani Iddi, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Said Bahanuzi,
Hamisi Kiiza/Frank Domayo na Nizar Khalfan/Didier Kavumbangu.source http://bongostaz.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment