Pambano la watani wa jadi Yanga
na Simba la Ligi Kuu ya Vodacom lililochezwa jana (Oktoba 3 mwaka huu)
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya bao 1-1
limeingiza sh. 390,568,000.
Watazamaji 50,455 walikata
tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa usiku kwa viingilio vya sh.
5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000 huku
kila klabu ikipata mgawo wa sh. 93,345,549.15 wakati Kodi ya Ongezeko la
Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 59,578,169.49.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni
posho ya msimamizi wa kituo sh. 240,000, kamishna wa mechi sh. 250,000,
waamuzi sh. 591,000, mwamuzi wa akiba (reserve referee) sh. 70,000,
usafi na ulinzi wa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (stadium technical
support) sh. 2,000,000.
Umeme sh. 750,000, maandalizi ya
uwanja (pitch preparation) sh. 400,000, ulinzi wa mechi sh. 5,860,000
wakati tiketi ni sh. 7,327,000. Gharama za mchezo sh. 31,115,183.05,
uwanja sh. 31,115,183.05, Kamati ya Ligi sh. 31,115,183.05, Mfuko wa
Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 18,669,109.83 na Chama cha Mpira
wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 12,446,073.22.
Wakati huo huo, mechi ya ligi
hiyo kati ya African Lyon na Toto Africans iliyochezwa Uwanja wa Azam
Complex na kushuhudiwa na washabiki tisa kwa kiingilio cha sh. 3,000
imeingiza sh. 27,000.
Mgawo wa mechi hiyo ulikuwa VAT
sh. 4,118.6 wakati kila timu ilipata sh. 6,864.3. Uwanja sh. 2,288.1,
gharama za mchezo sh. 2,288.1, Kamati ya Ligi sh. 2,288.1, FDF sh.
1,372.8 na DRFA sh. 915.2
No comments:
Post a Comment