Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, October 31, 2012

POLISI MORO WAAHIDI KUIUWA SIMBA LEO JAMHURI




MENEJA wa klabu ya Polisi Moro Sport Club na Msemaji wa klabu hiyo,
 Clement Bazo amesema kuwa klabu yake itaibuka na ushindi dhidi ya vinara 
wa ligi kuu ya vodacom Tanzania bara klabu ya Simba katika mchezo wao wa 
ligi hiyo utaopigwa leo kwenye uwanja wa Jamhuri majira ya saa 10:30 
mkoani hapa.

Bazo alisema kuwa mchezo huo utakuwa mchezo wao wa tisa tangu kuanza
 kwa ligi hiyo na kupoteza michezo sana na kutoa sare mbili na kujikusanyia 
pointi mbili wanauchukua mchezo huo kama michezo mingine baada ya
 kufanya vibaya hivyo lengo kuu ni kufanya vizuri na kuwa wamejindaa
 kukabiliana na vinara hao.

“Tumefanya maandalizi ya kutosha kwa michezo iliyobakia hivyo kesho
 (leo) tunacheza na Simba hivyo sisi Polisi lengo letu tulilonalo kwa sasa ni 
kufanya vizuri ukiwemo mchezo wetu dhidi ya dhidi ya Simba SC na 
tunaasilimia 75 ya ushindi kwa mchezo huo”. Alisema Bazo.

Bazo alisema kuwa mchezo ni mchezo matokeo ambayo yanahitajika katika
 mchezo huo kama watashindwa kuwafunga Simba basi mchezo utaweza 
kumalizika kwa sare ya aina yo yote ile.

Naye Kocha Mkuu wa klabu ya Polisi Sport Club, John Simkoko amesema 
maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Simba yamekabili na anachosubiri ni 
dakika 90 kuweza kuamua matokeo ya mchezo huo.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu kutoka jijini Dar es Salaam 
ambako wameweka kambi katika jeshi la polisi Kulasini, Simkoko alisema 
kuwa wachezaji wake wote wapo fiti kwa mchezo huo na anachosubiri ni 
kuanza kwa mchezo huo dhidi ya vinara wa ligi ligi Simba Sport Club hii leo.

Simkoko alisema kuwa waliweka kambi mapema katika jiji hilo baada ya
 mchezo wao dhidi ya Ruvu JKT kwa lengo kumalizia michezo iliyobakia 
ukiwemo na Simba katika uwanja wake wa nyumbani na kuwa 
dakika 90 ndizo zitakazoamua mshindi katika mchezo wa soka.
“Mchezo utakuwa mgumu kwa pande zote mbili na tumejiandaa vya
 kutosha kwa ajili ya kuikabili Simba hivyo najua Simba wanahitaji ushindi 
nasi vile vile tunahitaji ushindi katika mchezo huo lakini dakika 90 ndizo 
siku zote zinaamua matokeo ya mchezo ikiwemo sare, kupoteza na ”.
 alisema Simkoko.

Katika mchezo huo utanarajia kuibua hisia nyingine kutoka kwa mashabiki 
Manispaa ya Morogoro endapo klabu hiyo ya Polisi Moro kama itaendelea
 kupoteza mchezo huo baada ya kupoteza mwelekeo kufuatia kufungwa 
michezo saba na sare mbili huku ikiwa na pointi mbili

No comments:

Post a Comment