Stori kubwa Kenya ambayo hata kwenye leo ni kuhusu mamlaka ya mawasiliano nchini Kenya kuzizima kiteknolojia simu zote zilizofeki ambazo zimekua zikitumiwa na wakenya.Mtangazaji wa Citizen Tv/Radio William Tuva ameripoti kwamba wakenya walionunua simu feki wapo kwenye wakati mgumu na itawabidi wanunue simu original kwa sasa ili kurudi tena kwenye mawasiliano.Ameripoti pia kwamba inasemekana katika mtandao wa simu za mkononi wa Safaricom peke yake ni wateja laki sita ambao wameripotiwa simu zao kuzimwa kwa sababu ni feki.Mbali na hilo Tuva ameripoti pia kwamba Kenya imepoteza mabilioni ya shilingi kutokana na simu feki ambazo zimekua zikiingia sokoni kwa njia ambayo sio halali.Baadhi ya wananchi ambao simu zao zimefungwa wamekaririwa wakisema waliamka asubuhi na kukuta simu zao hazifanyi kazi, kumbe tayari zimeshazimwa kiteknolojia na tume ya mawasiliano nchini humo ambapo kwa mujibu wa BBC n wateja milioni mbili na nusu ambao simu zao zimezimwa.
Mmoja wa watu hao amekaririwa akisema “usiku ninawekaga alamu nataka saa 11 niamke, sikusikia naamka tu naona nje kunapambazuka na simu yangu wamezima"
WAZIRI WA FEDHA ASISITIZA UMUHIMU WA NCHI ZA AFRIKA KUTUNZA VYANZO VYA MAJI
ILI KUWA NA UCHUMI ENDELEVU
-
Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akichangia mada katika
mkutano ulioangazia umuhimu wa sekta ya maji katika maendeleo ya watu na
uchumi...
11 hours ago


No comments:
Post a Comment