WATU
watano wamekamatwa kwa makosa ya wizi wa umeme, wakitumia njia za
kuharibu mita na kujiunganishia huduma hiyo bila ya kufuata taratibu za
Shirika la Umeme nchini (Tanesco).
Msimamizi wa operesheni ya
ukaguzi wa mita uliyofanyika Temeke, Dar es Salaam juzi, Johari
Nasibu, aliwaeleza waandishi wa habari kuwa jumla ya nyumba 80
zilifanyiwa ukaguzi na baadhi ya hizo kukutwa na makosa hayo.
Alisema miongoni mwa makosa
waliyotwa nayo wateja hao watano ni pamoja na wizi kujiunginishia umeme
nje ya mita na kuchezea mita kwa kuziharibu ili ziweze kuandika
matumitumizi stahiki.
“Kama tunavyofanya siku zote
kwenye kazi hii leo hii tumefanya hapa Mtoni eneo la Relini,
tumefanikiwa kukuta mita nane zikiwa na makosa mbalimbali na hatua za
haraka tulizo zichukua ni kuwasitishia huduma kwanza kabla ya kufanya
tathmini ya hasara tuliyopata ili waweze kutulipa na kama hawajalipa
tunawafikisha mahakamani” alisema Nasibu.
Johari alisema kiasi kikubwa
cha umeme kimekuwa kikiibiwa na baadhi ya watu ambao siyo waaminifu
huku shirika hilo likiingia hasara bila kutarajia.
Aidha, shirika hilo linatarajia
kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale wote iwapo watabainika
mojamoja kwa moja na kujihusisha vitendo vya kulihujumu shirika hilo.
No comments:
Post a Comment