Kiongozi
wa Askari magereza, akiwaongoza Sheikh Ponda na wenzake, kutoka
mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, baada ya
kuahirishwa kwa kesi yao
Kiongozi
huyo mwenye msimamo mkali, alifikishwa kwa mara ya pili katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu pamoja na wafuasi wake ambapo hakimu
anayesikiliza kesi dhidi yake, Victoria Nongwa, ya kuvamia eneo la
Markaz, Chang'ombe jijini Dar es Salaam, ambapo waliharibu na kuiba
mali mbali mbali zenye thamani ya shilingi milioni 59, madai ambayo
washtakiwa wote waliyakanusha.
Hakimu
huyo alikubali kutoa dhamana kwa washtakiwa wote isipokuwa kiongozi
huyo ambaye ni mshtakiwa namba 1 kwa madai kuwa bado Mkurugenzi wa
Mashtaka nchini (DPP), hajaondoa pingamizi lake la kuzuia dhamana kwa
mshtakiwa namba moja.
Ulinzi
katika mahakama hiyo ulikuwa ni mkali na haujawahi kutokea katika miaka
ya hivi karibuni, ambapo pamoja na mambo mengine, palifungwa CCTV
Cameras, vifaa vya kugundua vitu vyenye asili ya chuma, polisi wa
kutuliza ghasia magereza na wale wa FFU, polisi wa farasi na mbwa,
pamoja na askari kanzu waliotapakaa kila kona ya maeneo ya jirani na
mahakama hiyo kubwa jijini Dar es Salaam.
Kikundi
kidogo cha wafuasi wa Sheikh Ponda, kilijaribu kuleta rabsha, lakini
polisi walitumia busara na kuwaelekeza kilichoamuliwa mahakamani ambapo
pamoja na kusuasua kuondoka eneo hilo la mahakama, lakini hatimaye
waliondoka huku polisi wa kutuliza ghasia wakiwafuata kwa nyuma hadi
eneo la makutano ya barabara za Bibi Titi na ile ya Morogoro nao
wakatawanyika.
Kwa
mujibu wa vyanzo vya uhakika vya habari, kulikuwepo taarifa kuwa wafuasi
hao walipanga kutega milipuko kwenye eneo la mahakama na pia
walisambaza vipeperushi vyenye vitisho kadhaa, ikiwa ni pamoja na
kufanya maandamano makubwa ya kulazimisha kiongozi huyo aachiliwe.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 15 mwaka huu itakapotajwa tena
|
No comments:
Post a Comment