Arusha
WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amekataa chakula Hoteli ya Mount Meru na kwenda kula chakula cha Mamalishe.
Tukio hilo lililowashangaza watu 13 waliokuwa katika msafara wake lilitokea hivi karibu wakati
WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amekataa chakula Hoteli ya Mount Meru na kwenda kula chakula cha Mamalishe.
Tukio hilo lililowashangaza watu 13 waliokuwa katika msafara wake lilitokea hivi karibu wakati
Profesa Muhongo alipokwenda Arusha kwenye mkutano wa wataalamu wa umeme wa nchi 11 za Afrika Mashariki, Kati na Kaskazini.
Waziri Muhongo aliandaliwa chakula hotelini hapo,
lakini aliwashangaza wenyeji wake ambao ni Shirika la Umeme Tanzania
(Tanesco) na uongozi wa wizara yake.
Baada ya kufika katika mgahawa wa Pizza Point
uliopo katikati ya mji wa Arusha, Waziri Muhongo aliagiza ugali na
samaki kwa bei ya Sh7,000.
Tukio la waziri huyo kukataa kula chakula cha
usiku katika hoteli hiyo ya kifahari, iliwashangaza hata wafanyakazi wa
mgahawa huo baada ya kupata taarifa hiyo.
Ingawa haikufahamika mara moja sababu za waziri huyo kukataa kula katika hoteli hiyo kutokana na kuchukua uamuzi ghafla, lakini taarifa za ndani zinadai hakutaka kutumia fedha za walipa kodi kwa matumizi binafsi.
Ingawa haikufahamika mara moja sababu za waziri huyo kukataa kula katika hoteli hiyo kutokana na kuchukua uamuzi ghafla, lakini taarifa za ndani zinadai hakutaka kutumia fedha za walipa kodi kwa matumizi binafsi.
“Waziri aliandaliwa chakula katika Hoteli ya Mount
Meru Arusha na mpaka tunatoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Kilimanjaro (Kia), ilijulikana tunakwenda kwenye hoteli hiyo lakini
chakushangaza alipofika karibu na geti la kuingia hapo, akabadili uamuzi
na kuamuru apelekwe mahali atakapopata chakula cha Kitanzania, huku
akisema haoni sababu ya kula vyakula vya bei mbaya wakati kuna
Watanzania hawana umeme,” alisema ofisa mmoja wa wizara hiyo ambaye
hakutaka kutajwa na kumkariri Waziri Muhongo:
“Nipelekeni mahali nitakapopata chakula cha
Kitanzania, ili tuwe sawa na Watanzania wenye hali ya chini kwani hizi
fedha tunazokwenda kula huko ni jasho lao.”
Hata hivyo, Profesa Muhongo anadaiwa kuruhusu
maofisa waliokuwa kwenye msafara wake ambao wangependa kula Mount Meru
kuwashusha, ili akitoka kwa mamalishe awapitie kwa sababu kila mtu ana
uamuzi wake.
Msafara wa waziri huyo ulikuwa na watu 13 akiwamo
Msaidizi wake na Meneja Mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud ambao wote
walilazimika kula chakula katika banda la Pizza Point.
Mmiliki wa mgahawa huo, Grace Lyatuu alisema
hakutarajia ujio wa waziri huyo na msafara wake, lakini baada ya
kutambua kuwa ni Profesa Muhongo akamshukuru Mungu kwa kumfikisha hapo.
“Kwakweli ilikuwa ni usiku mgumu kwangu, kwani
msafara ulikuwa mkubwa na wagafla, sikuwa na uhakika wa kupata vyakula
vya kuwatosha lakini baada ya chakula kupatikana nikamshukuru Mungu
kwani ilikuwa ni usiku na tulikuwa na maandalizi ya kufunga mgahawa,”
alisema Lyatuu.
Profesa Muhongo alitumia Sh100,000 kwa chakula cha watu 13 na vinywaji na kuokoa zaidi ya Sh344,500.
No comments:
Post a Comment