
Wote
tunafahamu kuwa aliyekuwa gavana wa benki kuu ya Tanzania Daudi Balali
alifariki dunia tarehe 16.05.2008 huko Boston, Marekani na kuzikwa huko
huko.
Lakini
kwa watumiaji wa Twitter watakuwa wanamfahamu Daudi Balali wa kwenye
mtandao huo ambaye ameendelea kumuumiza vichwa vya watu wengi kuwa ni
nani huyu aliye nyuma ya akaunti hiyo na akiendelea kudai kuwa bado yupo
hai?
October 1 alitweet, “Nitakutana na Rais Kikwete na ujumbe wake wiki hii hapa Marekani.
Anavyoonekana ni msomi haswaa na
anaishi nje ya nchi. Ni mtu makini, ana hoja, anaijua siasa ya Tanzania
na yupo consistent! Hivi karibuni mtu huyo alidai kuwa amekuja Tanzania
na kulala kwenye hoteli iliyo karibu na ofisi yake ya zamani.
“In
Dar es Salaam, Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kempinski Kilimanjaro
Hotel. Feels good to be close to my former office, BoT,” alitweet
November 13.
Kutokana
na kile anachokiandika anaonekana kuwa ni kada mzuri wa CCM na leo
ameibuka na kutabiri anguko la CHADEMA kwa kutweet, “Chadema will die by
disintegration. Zitto Kabwe and 3 other prominent members will move to
CCM,the rest will form 2 new political parties.
Anasema
CHADEMA itavunjika ambapo Zitto Kabwe na wanachama wengine watatu wa
chama hicho watahamia CCM na wengi wataanzisha vyama viwili vipya vya
siasa.
Hata hivyo anadai ameamua kuondoka nchini mapema na kurudi Gaithersburg, Maryland kutokana kuhofia usalama wake.
“I am leaving Dar es Salaam tonight instead of Wednesday on security reasons.”
Mwisho ameendelea kusisitiza kuwa kweli yupo hai kwa kutweet:
I AM REAL. TAKE IT OR LEAVE IT. TWITTER IS THE MESSENGER. THE SURPRISE IS YET TO COME.
Ni nani huyu? Anyways, wonders will never cease!

No comments:
Post a Comment