
Paroko wa
Parokia ya Isimani, Baba Anjelo Burgo akiwa kitandani kwenye chumba
maalumu katika Hosptali ya Mkoa wa Iringa wakti akisubiri kufanyiwa
upasuaji kwa lengo la kutoa risasi zilizosalia mwilini baada ya watu
wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha za jadi na Bunduki
kuvamia nyumba wanazoishi mapadri usiku wa kuamukia jana. Picha na Said
Ng’amilo.
MAPADRI
wawili wa Kanisa Katoliki Parokia ya Isimani, Jimbo la Iringa,
wamejeruhiwa vibaya na kulazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa,
kutokana na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi kuwajeruhi kwa silaha za
jadi na bunduki, baada ya kuvamia nyumba wanazoishi.
Paroko wa
Kanisa hilo Angelo Burgio kutoka Italia (60) na msaidizi wake Herman
Myala walikumbwa na mkasa huo usiku wa kuamkia jana.
Padri
Burgio alijeruhiwa kwa kupigwa risasi mbili kifuani na kucharangwa
mapanga, msaidizi wake Padri Myala alijeruhiwa kwa mapanga na kuburutwa
chini kwenye ardhi.
Tukio
hilo limetokea ikiwa ni siku moja tangu kuvamiwa kwa Kanisa Katoliki
Jimbo la Iringa lililopo eneo la Kihesa mkoani humo, ambapo mlinzi wa
kanisa hilo, Batholomea Nzigilwa (65) alijeruhiwa na kitu chenye ncha
kali kichwani.
Nzigilwa amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa, huku hali yake ikielezwa ikiwa ni mbaya.
Watangaza msamaha.
Jana gazeti hili lilishuhudia Padri Burgio akiwa amelazwa, huku akiwa ametundikiwa chupa ya maji wakati akisubiri huduma ya upasuaji kwa ajili ya kutolewa risasi mwilini.
Jana gazeti hili lilishuhudia Padri Burgio akiwa amelazwa, huku akiwa ametundikiwa chupa ya maji wakati akisubiri huduma ya upasuaji kwa ajili ya kutolewa risasi mwilini.
Akizungumza
kwa tabu, padri huyo alisema majambazi hao walifika eneo la Kanisa la
Kihesa saa tano usiku wakiwa na silaha mbalimbali za jadi na bunduki.
Alisema baada ya kumshambulia msaidizi wake, walimfyatulia yeye risasi kifuani wakati alipofungua mlango na kutaka kukimbia.
“Mimi
baada ya kuwasikia nilifungua mlango kwa lengo la kutaka kukimbia ili
nijinusuru, lakini hamadi wakanifyatulia risasi kifuani.
Nilianguka
chini na walipoingia ndani walichukua fedha taslimu Sh3.5 milioni
zilizokuwa chumbani kwangu na kisha kunikata na panga kichwani, ”
alisema Burgio.
Hata
hivyo, padri huyo alisema, “Sisi tunawasamehe. Mimi na mwenzangu
tumewasamehe tangu walipofanikiwa kutushambulia na kukimbia. Tunawaombea
msamaha kwa Mungu kwani yeye ndiye anayejua,” alisema Padri Burgio.

No comments:
Post a Comment