Waasi
nchini Jamuhuri ya Kidemokrasi ay Congo, wamepuuzilia mbali wito kutoka
kwa viongozi wa kimataifa wa kusitisha mapigano na pia kuondoka kutoka
mji wa Goma Mashariki mwa nchi hiyo.
Msemaji
wa kundi hilo la waasi wa M23, amesema wapiganaji wao wataendelea na
mapigano hayo hadi pale serikali ya rais Joseph Kabila itakapokubali
kutekeleza masharti yao.
Awali
rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, alisema yuko tayari
kuchunguza malalamishi ya wapiganaji wa waasi ambao wameuteka mji wa
Goma, Mashariki mwa nchi hiyo.
Akiongea
baada ya mazungumzo yaliyofanyika nchini Uganda na Kuhudhuriwa na rais
wa Rwanda, Paul Kagame, Rais Joseph Kabila amesema anatathmini uwezekano
wa kuanzisha mazungumzo na waasi hao wa M23.
Mwenyekiti
na mwenyeji wa Mazungumzo hayo, rais wa Uganda Yoweri Museveni, rais
Kabila na Kagame kwa kauili moja walitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano
hayo na pia kutoa amri kwa waasi hao kuondoka Goma mara moja.
Wapiganji hao wa waasi wametishia kuendeleza mapigano hayo hadi mji mkuu wa nchi hiyo Kinshasa.
Mazungumzo ya amani
Wakati huo huo, ripoti zinasema kuwa rais wa M23 yuko njiani kuelekea mjini Kampala kwa mazungumzo na rais YowerI Museni.
Rais
Museveni, ameitisha kikao na viongozi wa waasi hao ili kujadili harakati
za kumaliza mzozo huo Mashariki mwa Congo, na yametokea siku moja tu,
baada ya rais huyo wa Uganda kufanya mashauriano mengine na rais Kabila
na mwenzake kutoka Rwanda Paul Kagame.
Hapo jana, wapiganaji hao wa M23 waliuteka mji wa Sake, ulioko takriban kilomita 27, kutoka Goma.
Ripoti zinasema wapiganaji hao sasa wanajiandaa kuelekea eneo la Kusini hadi Bukavu, takriban kilomita 230 kutoka Goma.
Kamanda
mmoja wa waasi hao, aliliambia umati wa watu waliokusanyika katika
uwanja wa michezo mjini Goma, kuwa safari yao ya kukomba taifa hilo
imeanza.
Lakini mwandishi wa mjini Goma, anasema haijabainika wazi ikiwa wapiganaji hao wa waasi wana uwezo wa kutekeleza vitisho vyao.
Lakini mwandishi wa mjini Goma, anasema haijabainika wazi ikiwa wapiganaji hao wa waasi wana uwezo wa kutekeleza vitisho vyao.
Kundi hilo la M23 liliundwa mwezi April mwaka huu baada ya wanajeshi kadhaa kuasi.
Wapiganaji hao wa waasi wanasema hawakupewa nyadhifa za kijeshi walizohaidiwa baada ya kusainiwa kwa mkataba wa amani mwaka wa 2009.
Wapiganaji hao wa waasi wanasema hawakupewa nyadhifa za kijeshi walizohaidiwa baada ya kusainiwa kwa mkataba wa amani mwaka wa 2009.
Vitendo
vya wapiganaji hao wa M23, vimezua wasi wasi wa kuzuka upya kwa mapigano
nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambako takriban watu milioni
tano waliauawa kufuatia mapigano yaliyoanza mwaka wa 1997 na kumalizika
mwaka wa 2003.
No comments:
Post a Comment