Ripoti  ya Umoja  wa  Mataifa imeonyesha kuwa idadi  ya  watu   wapya walioambukizwa  virusi vya ukimwi imepungua  kwa asilimia  22  kati  ya  mwaka  2001  na  2011.
Ripoti  hiyo ambayo ilifanyiwa  uchunguzi  na  Mpango  wa  Pamoja wa  Umoja  wa  Mataifa kuhusu  ukimwi  na  HIV, imegundua kuwa  idadi  ya  vifo  vinavyohusiana  na  ugonjwa  wa ukimwi  imepungua  katika  miaka  kumi  iliyopita.
Ripoti hiyo  imesema  kuwa  matokeo  hayo  ni  kwa  upande fulani  kutokana  na  upatikanaji  kwa  wingi  wa  dawa  za kuzuia watu  walioambukizwa  virusi  vya ukimwi, lakini  imesema  pia  kuwa  kazi  kubwa  zaidi  inapaswa kufanywa.
Mwaka  jana lengo  lilikuwa kupunguza kwa nusu  idadi ya maambukizi ya kila mwaka ya HIV ifikapo  mwaka  2015.