Na Zitto Kabwe
GAZETI la The East African la Novemba 24 – 30, 2012 limetoa taarifa kwamba jumla ya dola za kimarekani milioni 54 zimegundulika kuibwa na watumishi waandamizi wa Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la TANESCO kupitia manunuzi ya Mafuta ya kuendesha mtambo wa Umeme wa IPTL.

Gazeti
hili limenukuu taarifa ya ukaguzi kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Tanzania (Controller and Auditor General). Taarifa hiyo inasema kuna
kikundi (racket) ambacho kazi yake kubwa ni kujifaidisha binafsi na
mpango wa umeme wa dharura kupitia manunuzi ya Mafuta mazito ya IPTL.
Itakumbukwa
kwamba toka mwaka 2011 kumekuwa na shinikizo lililotolewa na Kamati ya
Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Kamati ya Bunge ya Nishati na
Madini na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini kwamba zabuni za ununuzi wa
mafuta ya kuendesha mpango wa umeme wa dharura na mchakato mzima wa
manunuzi ya mafuta haya ufanyiwe uchunguzi wa kina (forensic audit).
Katika
mkutano wa 3 wa Bunge la Kumi (April 2011) niliuliza swali Bungeni
kuhusu kashfa hii ya ununuzi wa mafuta ya kuendesha mtambo wa IPTL na
baadaye tarehe 16 Aprili 2011 nilimwomba Spika airuhusu Kamati ya
Nishati na Madini kufanya uchunguzi kuhusu kashfa hii.
Kamati ya
Nishati na Madini chini ya aliyekuwa Mwenyekiti ndugu January Makamba
ililitaka Bunge kuazimia kufanyika kwa uchunguzi kuhusu suala hili
kwenye Taarifa yake ya mwaka 2011 iliyowasilishwa Bungeni mwezi Aprili
mwaka 2012. Waziri Kivuli wa Nishati na Madini ndugu John Mnyika katika
Hotuba yake ya Bajeti ya Wizara hiyo mwaka 2011 alipendekeza kufanyika
kwa uchunguzi kuhusu kashfa hii pia. Juhudi zote hizo hazikuzaa matunda.
Kipindi hicho kiwango kilichokuwa kinahojiwa kuibwa ni shilingi bilioni 15 tu. Taarifa ya The East African kama walivyonukuu kutoka kwenye taarifa ya CAG inaonyesha fedha zilizoibwa ni shilingi bilioni 86.
Zabuni za kununua mafuta ya kuendesha umeme wa dharura zimekuwa zikitolewa bila kufuata utaratibu wa zabuni kwa mujibu wa Sheria ya manunuzi.

Hivi sasa
kila mwezi Tanzania inatumia dola milioni 70 kununua mafuta ya
kuendesha mitambo ya umeme. Fedha hizi zinatoka Hazina na sehemu ndogo
kutoka TANESCO. Wakati fedha hizi bilioni 112 zinachomwa kila mwezi
kununua mafuta mazito na dizeli ya kuendesha mitambo ya umeme, Taarifa
za kitaalamu zinaonyesha kwamba Bwawa la Mtera hivi lina kina cha maji
chini ya kiwango kinachotakiwa na uzalishaji wa umeme ni asilimia 20 tu
ya uwezo (installed capacity).
Iwapo
TANESCO wataendelea kutumia zaidi maji yaliyopo Mtera, Mitambo
itashindwa kazi na Gridi nzima itasimama maana Mtera ndio nguzo kuu ya
Gridi ya Taifa. Hali hii ni hatari sana kwa uchumi na ulinzi na usalama
wa Taifa. Kimsingi Gridi ya Taifa ipo hatarini kutokana na kiwango cha
Maji kilichopo Mtera hivi sasa na kuendelea kupungua kwa kina hicho cha
maji.
Wananchi wanapaswa kuelezwa kinaga ubaga nini kinaendelea katika sekta ndogo ya umeme hapa nchini;
1. Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali kuhusu zabuni za manunuzi ya Mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme wa dharura iwekwe wazi na ‘racket’ inayosemekana kuiba jumla ya shilingi bilioni 86 ionyeshwe na hatua za kisheria zichukuliwe mara moja na bila kuchelewa.

2. Waziri
wa Nishati na Maadini auleze umma hali yalisi ya sekta ya umeme nchini,
uzalishaji wa umeme upoje, hali ya maji katika bwawa mkakati la Mtera
na nini hatma ya mitambo ya IPTL, kesi zake na utekelezaji wa
mapendekezo ya Bunge kuwa kesi za kampuni hii zimalizwe nje ya mahakama.
Pia Taifa lielezwe Mpango wa Dharura wa umeme unakwisha lini maana muda
uliotolewa na Bunge mwezi Agosti mwaka 2011 tayari umekamilika. Waziri
aeleze hatua agni amechukua baada ya kukabidhiwa taarifa na CAG kuhusu
maafisa waandamizi wa Wizara waliohusika na wizi wa shilingi bilioni 86
za kununua mafuta ya IPTL.
3. Waziri
wa Fedha na Uchumi aueleze umma ni kiwango gani cha fedha Hazina imetoa
kununua mafuta ya kuendesha mitambo ya umeme wa dharura kati ya Mwezi
Novemba mwaka 2011 na Oktoba mwaka 2012 na kama taratibu zote za zabuni
zilifuatwa na pale ambapo hazikufuatwa ni hatua gani PPRA wamechukua
dhidi ya waliokiuka sheria ya manunuzi na kuleta hasara ya mabilioni ya
fedha kwa Serikali.
No comments:
Post a Comment