Hivi
ndivyo ilivyokuwa katika zulia jekundu la EBSS ndani ya Ukumbi wa
Diamond Jubelee Usiku wa Novemba 9 2012. Watu walishine vilivyo ama
kulipuka na swaga zao kiabo
WALTER CHILAMBO NDIYE MSHINDI WA EBSS 2012
Mshindi
wa shindano la Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS),Walter Chilambo
(Dar) akikabidhiwa sanduku lake lenye kitita cha shilingi milioni 50
jana usiku ndani ya ukumbi wa Diamond jubilee,katika shindano hilo
lililovuta hisia za wengi,mshindi wa pili ameibuka mwanadada Salma
Abushiri (Zanzibar) na watu ni Wababa Mtuka (Dar)
Mshindi
wa shindano la Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS),Walter Chilambo
(Dar) akiwashukuru wapenzi na msahabiki wake waliompigia kura na
hatimaye kuibuka mshindi wa shindano hilo,lililofanyika ndani ya ukumbi
wa Diamond jubilee,
Baadhi
ya mashabiki wa mshindi wa shindano hilo la EBSS,Walter Chilambo
wakishangilia kwa shangwe na vifijo mara baada kutamkwa yeye ndiye
kinara katika kilele cha shindano hilo lililovuta hisia za watu wengi
Mkurugenzi
wa kampuni ya Benchmark Productions Limited, na jaji mkuu wa Shindano
la Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS), akiwa amemkumbatia mshindi wa
shindano hilo Walter Chilambo ndani ya ukumbi wa Diamond,Chilamba
ameibuka na kitita cha shilingi Milioni 50
Msanii Barnaba akiimba na mmoja wa washiriki wa shindano la Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS),
Mshiriki wa EBSS NshomaNg'hangasamala akiimba moja ya wimbo wake jukwaani.
Mwanadada
Salma Albushiri akiimba kwa hisia huku akipiga gitaa mbele ya mashabiki
wake waliofika kumshuhudia ndani ya ukumbi wa Diamond usiku huu.
Mapouda.! majaji hawaishi vituko
Mashabiki kama kawa.
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Linah na Amin wakiimbwa kwa pamoja wimbo mpya uitwa Mtima Wangu
Mwasiti akicheza na Wababa
WALTER
CHILAMBO ndiye mshindi wa Shindano la Epic Bongo Star Search (EBSS)
2012. Kufuatia matokeo hayo Kalambo amejinyakulia kitita cha Shilingi
Milioni 50 za Kitanzania kutoka kwa wadhamini wakuu wa shindano hilo
kampuni ya Simu za Mkononi ya Zantel.
Chilambo
ametwaa ubingwa huo baada ya kumwangusha mwana dada kutoka Zanzibar
ambaye alikuwa ni mshindani wake wa karibu katika kinyang’anyoro hicho
Salma Yusufu.
Salma Yusufu
Shindano
la EBSS usiku huu limefikia patamu baada ya washiriki 3 walio ingia
katika fainali hizo kutoka na sasa kubakia washiriki wawili ambao ni
Walter Chilambo na Salama Yusufu mwakilishi pekee kutoka kisiwani
Zanzibar.
Washiriki
waliotoka usiku huu na kuachia kitita chaa Shilingi Milioni 50,
kikiwaniwa na Walter na Salama ni pamoja na Nsami Nkwabi, Nshoma
Ng’hangasamala Wababa Mtuka.
Shindano la EBSS linafikia tamati yake usku huu katika ukumbi wa Diamond Jublee linapoendea kufanyika.
Kama kawaida nao hutoa burudani ....Chief Jaji na mratibu wa Shindano la Epiq Bongo Star Search (EBSS), Mkurugenzi wa kampuni ya Benchmark Productions Limited,
Ritha Poulsen a.k.a Madam Ritha, akifurahia jambo wakati washiriki
wakitumbuiza jukwaani. Kulia ni Jaji mwingine Master Jay akionekana kama
kukera na kicheko cha Madam Ritha.
Mashabiki
na wapenzi wa shindano la Epiq Bongo Star Search (EBSS) waliofurika
katika ukumbi wa Diamond Jubelee wakilipuka kwa shangwe baada ya mmoja
wa washiriki ambao wanamkubali kumaliza kufanya show yake.
No comments:
Post a Comment