Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, November 19, 2012

USHIRIKINA UPO JAMANY;ANGALIA PICHA NAMNA BIBI KIZEE ALIVYODONDOKA NA UNGO MITAA YA KINONDONI KWA MAMBO YAKE YA USHIRIKINA!




BIBI AJIELEZA, AJICHANGANYA
Bibi huyo, akiwa amezingirwa na umati wa wananchi wenye hasira kali, alipotakiwa ajieleze alikotokea, alijichanganya kwani jibu lake la kwanza alidai ameanguka kutoka angani akitokea Tabora.
Alipozidi kubanwa kwa maswali, alibadili kauli na kusema alianguka akiwa safarini kutokea Tanga, kauli zilizowapandisha hasira wananchi wenye imani potofu za ushirikina, wakiongozwa na dada mmoja aliyejitangaza kuwa amepandisha mashetani na kudai eti bibi huyo ni mwanga kwa mujibu wa mashetani yake.


MASHETANI YACHOCHEA HASIRA
Mashetani ya dada huyo yalizidi kuwaongeza hasira wananchi hao wenye imani za kishirikina ambao walianza kukusanya vitambaa na makaratasi ya maboksi huku wengine wakianza kutafuta mafuta ya taa ili wamwagie kisha wamchome moto bibi kizee huyo, ndipo walipotokea wasamaria wema waliomuokoa na Kumpelea polisi.
POLISI WANENA
Kufuatia tukio hilo, siku iliyofuata mwanahabari wetu alifika kituo cha polisi alichokimbizwa bibi huyo ili kupata ukweli zaidi ambapo askari mmoja aliyekutwa kituoni hapo, aliyeomba jina lake lisiandikwe kwenye mitandao kwa kuwa siyo msemaji wa jeshi hilo, alikiri kupokelewa kwa kikongwe huyo.
“Ni kweli bibi huyo aliletwa hapa kituoni saa tisa usiku lakini kulikuwa hakuna kosa lolote la jinai tuliloona kuwa anastahili kufunguliwa mashitaka. Jeshi la polisi haliamini ushirikina, baada ya watu kutawanyika na kuona kuna usalama tulimuachia, tumefarijika kuona wananchi hawakujichukulia sheria mikononi, waendelee kufanya hivyo.” alisema askari huyo

1 comment:

  1. wangemchoma 4 sure so kaanguka na walitegemea kaanguka from heaven au??? wangemchoma tuu

    ReplyDelete