April 5, 2012
GODBLESS LEMA AVULIWA KITI CHA UBUNGE ARUSHA MJINI
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini (CHADEMA), Godbless Lema.
Kesi
hiyo iliyofunguliwa na makada watatu wa CCM, Agness Mollel, Mussa
Mkanga na Happy Kivuyo ambao walikuwa wanamtuhumu mbunge huyo kwamba
alitoa kauli za udhalilishaji, matusi na kashfa kwa aliyekuwa mgombea wa
ubunge jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Edelea kufuatilia audifacejackson blogspot.Dk Batilda Burianimetolewa hukumu na jaji Gabriel Rwakibarila.
April 13, 2012
DKT JK AWAAPISHA WAJUMBE WA TUME YA KURATIBU MAONI YA WANANCHI KUHUSU KATIBA MPYA IKULU.
Rais
Jakaya Kikwete akizungumza na Makamu wa rais, Dkt, Mohamed Ghalib
Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein na Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda katika sherehe za kuwaapisha wajumbe wa Tume ya kuratibu Maoni
ya Wananchi Kuhusu Kuundwa kwa Katiba Mpya zilizofanyika Ikulu jijini
Dar es salaam Aprili 13,2012.
Rais
Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Tume ya
Kuratibu Moani ya Wananchi Kuhusu Kuundea kwa Katiba Mpya baada ya
kuwaapisha, Ikulu jijini Dar es salaam, Aprili 13, 2012. (Picha zote na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
April 30, 2012
Mahakama Yamvua Ubunge Mbunge Sumbawanga Mjini ( CCM)
Hukumu
ya kupinga matokeo ya ubunge wa sumbawanga mjini wa Aeshy Hilaly
Halphany CCM dhidi ya mwalimu Norbet Joseph Yamsebo wa Chadema ambaye
anadai kuchakachuliwa katika uchaguzi huo.Edelea kufuatilia audifacejackson blogspot.Madai
miongoni ni pamoja na kutoa rushwa kwa makundi mbalimbali na watu wengi
walijitokeza kutoa ushahidi huo na kukiri kuwa ni kweli walipokea vitu
mbalimbali ikiwemo fedha, baskeli, pikipiki, vinywaji, kinanda kwa
kanisa katoliki, nk kwa sharti la kumpigia kura mbaya zaidi ni kwa
mkurugenzi mwanamama kutoa ushahidi wa kupinga ushindi wa mbunge huyo,
mkurugenzi huyo alihamishwa muda mfupi mara baada ya matokeo ya uchaguzi
kutolewa na kupelekwa wilaya ya Ileje.
BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI MEI 2012 HILI HAPA
Rais
Jakaya Kikwete hivi punde ametangaza Baraza jipya la Mawaziri likiwa na
sura mpya wakati baadhi ya Mawaziri wakibaki katika nafasi zao.
Ifuatayo ni orodha ya Mawaziri na Manaibu walioteuliwa.
HII NDO ORODHA NZIMA YA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI MAWAZIRI
1. OFISI YA RAIS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Ndugu Stephen M. Wasira, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora) Ndugu George Mkuchika, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (UTUMISHI) Ndugu Celina Kombani, Mb.,
2. OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MUUNGANO) Ndugu Samia H. Suluhu, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MAZINGIRA) Dr. Terezya P.L. Huvisa, Mb.,
3. OFISI YA WAZIRI MKUU
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Ndugu Mary M.
Nagu, Mb., Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Ndugu Hawa
Ghasia, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Ndugu William V. Lukuvi, Mb.,
4. WIZARA
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Ndugu Samuel J. Sitta, Mb.,
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ndugu Shamsi Vuai Nahodha, Mb.,
Waziri wa Ujenzi Dr. John P. Magufuli, Mb.,
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hussein A.H. Mwinyi, Mb.,
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr. Shukuru J. Kawambwa, Mb.,
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ndugu Sophia M. Simba, Mb.,
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Ndugu Bernard K. Membe, Mb.,
Waziri wa Katiba na Sheria Ndugu Mathias M. Chikawe, Mb.,
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Ndugu Emmanuel Nchimbi, Mb.,
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dr. David M. David, Mb.,
Waziri wa Kazi na Ajira Ndugu Gaudentia M. Kabaka, Mb.,
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame M. Mbarawa, Mb.,
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna K. Tibaijuka, Mb.,
Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe, Mb.,
Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum Prof. Mark Mwandosya, Mb.,
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Eng. Christopher Chiza, Mb.,
Waziri wa Uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe, Mb.,
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dr. Fenella E. Mukangara, Mb.,
Waziri wa Maliasili na Utalii Ndugu Khamis Kagasheki, Mb.,
Waziri wa Viwanda na Biashara Dr. Abdallah O. Kigoda, Mb.,
Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa, Mb.,
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo, Mb.,
5. NAIBU MAWAZIRI OFISI YA RAIS
HAKUNA NAIBU WAZIRI
6. OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais Ndugu Charles Kitwanga, Mb.,
7. OFISI YA WAZIRI
Naibu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Ndugu Majaliwa K.
Majaliwa, Mb., Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Aggrey Mwanry, Mb.,
8. WIZARA MBALIMBALI
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Dr. Makongoro M. Mahanga, Mb.,
Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Ndugu Adam Malima, Mb.,
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Ndugu Pereira A. Silima, Mb.,
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Ndugu Gregory G. Teu, Mb.,
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Ndugu Benedict N. Ole-Nangoro, Mb.,
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Ndugu Mahadhi J.
Maalim, Mb., Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ndugu
Goodluck J. Ole-Medeye, Mb., Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia
na Watoto Ndugu Ummy A. Mwalimu, b.,
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Ndugu Philipo A. Mulugo, Mb.,
Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Abdulla Juma Abdulla, Mb.,
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Ndugu Lazaro Nyalandu, Mb.,
Naibu Waziri wa Ujenzi Ndugu Gerson Lwenge, Mb.,
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dr. Seif Suleiman Rashid, Mb.,
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Ndugu George Simbachawene, Mb.,
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Ndugu January Makamba, Mb.,
Naibu Waziri wa Uchukuzi Dr. Charles J. Tizeba, Mb.,
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Ndugu Amos Makala, Mb.,
Naibu Waziri wa Maji Eng. Dr. Binilith Mahenge, Mb.,
Naibu Waziri Nishati na Madini Ndugu Stephen Maselle, Mb.,
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Ndugu Angela Jasmine Kairuki, Mb.,
Naibu Waziri wa Fedha Ndugu Janet Mbene, Mb.,
Naibu Waziri wa Fedha Ndugu Saada Mkuya Salum,
May 24, 2012
JOHN MNYIKA ASHINDA KESI YAKE
Mbunge
wa jimbo la Ubungo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA
John Mnyika ameshinda kesi yake iliyofunguliwa na aliyekuwa Mgombea
kupitia chama cha Mapinduzi CCM Bi.Hawa Ngh'umbi. Kesi hiyo iliyokuwa
ikiendeshwa katika mahakama kuu imempa ushindi bwana Mnyika. Wakiwa
wamembeba kwa furaha kubwa wafuasi wa CHADEMA walisikika wakiimba kwa
sauti kubwa PEOPLES POWER
Mbunge CCM Akamatwa Kwa Rushwa
Mbunge wa Jimbo la Bahi (CCM), Omary Badwel
Neville Meena na Fidelis Butahe
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) inamshikilia Mbunge wa Jimbo la Bahi (CCM), Omary Badwel kwa tuhuma za kupokea rushwa ya Sh1 milioni kutoka kwa kiongozi wa Serikali.Edelea kufuatilia audifacejackson blogspot.Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa taasisi hiyo, Alex Mfungo zinaeleza kuwa Badwel alikamatwa na maofisa wa Takukuru jana saa 9:00 alasiri katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
Badwel ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) anadaiwa kukamatwa wakati anapokea rushwa kutoka kwa maafisa wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani jana.
Mfungo aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa wanaendelea kumshikilia huku wakati wanafanya uchunguzi hadi kesho ambapo watamfikisha mahakamani.
“Siwezi kumataja aliyekuwa akitoa rushwa kwa sababu bado tunaendelea na upelelezi, ila mpaka sasa yuko mahabusu na tutamfikisha mahakamani Jumatatu(kesho),” alisema Mfungo.
Alisema kuwa mbali na kumfikisha mahakamani, pia watatoa taarifa zaidi za tukio hilo kesho.
june 26
DR ULIMBOKA ATEKWA, APIGWA, HALI YAKE MBAYA SANA MOI
Kiongozi
wa jumuiya ya kushughulikia matatizo ya madaktari Dr Stephen Ulimboka
hapo jana majira ya saa sita usiku alitekwa, kupigwa na watu watatu
wenye silaha na kisha kutupwa maeneo ya mabwepande ambapo aliokotwa na
kupelekwa katika taasisi ya mifupa (MOI) jijini Dar-es-salaam.
Dr
Ulimboka, ambaye kamati yake ndio inaratibu na kuongoza mgomo wa
madaktari, alipigiwa simu na mtu anayejiita “Abeid” ambaye
alijitambulisha kama afisa wa serikali aliyetaka waonane uso kwa uso ili
kutafuta suluhu baina ya serikali na madaktari ambao kwa sasa wapo
kwenye mgomo nchi nzima.
Hali
ya kiongozi huyo wa jumuiya ya mpito ya madaktari inasemekana ni mbaya
sana na maombi ya watanzania wote yanahitajika kwa sasa.
Wakati
taarifa hizi zikiwa zimegaa na kuzua taharuki kwa madaktari wote pamoja
na wananchi, madaktari bado wameendelea na msimamo wao wa kugoma na
kuapa kutorudi nyuma katika kutetea maslahi yao, mazingira bora ya kazi,
vitendea kazi vizuri, pamoja na kuitaka serikali kutoa kipaumbele
kwenye suala la afya ya mwananchi ili waweze kutoa tiba iliyobora na
hivyo kuwahudumia watanzania wote kwa ufasaha zaidi.Edelea kufuatilia audifacejackson blogspot.Tutaendelea
kuwaletea habari zaidi kuhusu kiongozi huyu wa jumuiya ya madaktari
.MUNGU amjaalie apone haraka ili aendeleza kutetea maslahi ya
madaktari na wananchi wote kwa jumla.
July 19, 2012
No comments:
Post a Comment