Baadhi ya wachezaji wa timu ya Mpira wa magongo
(HOCKEY) Zanzibar wakiisubiri timu ya wazee kwa ajili ya mechi
iliyoandaliwa na chama cha mpira huo huko katika uwanja wa Mau.
Mwandishi wa habari kutoka chuchu FM Redio Yahya Saleh
akimuhoji kocha wa timu ya mpira wa magongo (HOCKEY) Mgeni Haji juu ya
upatikanaji wa vifaa vya mchezo huo ambapo alisema ni ghali mno.Timu ya wachezaji wa zamani wa magongo (HOCKEY) wakiwa katika mapumziko mafupi (Halftime)huko katika uwanja wa Mau.
Mchezaji wa timu ya Kombaini Halifa Abdallah Maabadi mwenye bukta ya njano akisawazisha bao katika mechi hiyo ambayo ilitoka mbili mbli.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar
Na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar 28/12/2012
Makamo
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa magongo (HOCKEY) Zanzibar Ramadhan
Pandu Makame ameiomba Serekali pamoja na wadau wa Michezo kusaidia
upatikanaji wa vifaa vya mchezo huo ili waweze kuuendeleza na kushiriki
katika mashindano ya ndani na nje ya nchi.
Ramadhan
ameyasema hayo katika Bonanza la Mchezo huo lililoandaliwa na chama
hicho kwa lengo la kujindaa na mashindano ya Mapinduzi Cup
yanayotarajiwa kufanyika jijini Dar es laam Januari 09 mwakani.
Amesema
Vifaa vya mchezo wa Mpira wa Magongo ni ghali sana kiasi cha wao
kushindwa kumudu kuvinunua na hivyo kulazimika kuomba msaada ili
wasaidiwe kupatikana kwake.
Ameongeza
kuwa Zanzibar kuna vipaji lukuki vya mchezo huo lakini kinachokosekana
ni vifaa na ushajihishwaji wa vijana kujiunga na mchezo huo.
Ramadhan
amedai kuwa kama kutakuwa na ushirikiano wa kutosha na kuwezeshwa
kikamilifu chama hicho anaamini kuwa Zanzibar inaweza kuwa na timu
zinazoweza kufanya vizuri katika mashindani ya kitaifa na kimataifa.
Akizungumzia
kuhusu mashindano ya Mapinduzi Cup Ramadhan amesema mashindano hayo
yatazishirikisha timu nane ikiwemo timu ya Zanzibar.
Kwa
upande wao Wachezaji wakongwe wa Mpira wa magongo wamekipongeza chama
cha mpira huo kwa kuandaa mechi kati yayo na timu ya kombaini ya
Zanzibar ikiwa pamoja na kuwashajihisha vijana ili kuupenda mchezo huo.
Aidha
wamekishuri Chama hicho kuandaa mechi za mara kwa mara kati yao ili
kuipa ukomavu timu hiyo na pia kuutangaza mchezo kwa Wazanzibari
Katika
Bonanza hilo Timu ya Maveterani wa mchezo huo ilipimana nguvu na Timu
ya Kombaini ya JWTZ na KMKM ambapo matokeo ya mchezo huo ni suluhu ya
mabao mawili kwa mawili.
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment