Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, January 12, 2013

Angalia Trailer ya Movie inayohusu machafuko yaliyotokea Kenya baada ya uchaguzi wa mwaka 2007, inaitwa "Something Necessary"

Miaka kadhaa imepita baada ya Kenya kukumbwa na balaa la machafuko yaliyopelekea vifo vingi vya watu, majeraha ya kudumu na watu wengi kukosa makazi yao baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 (post election violence). Wasanii wa maigizo nchini humo wameshafanya filamu inayohusu matukio yaliyotokea wakati huo na filamu inaitwa "Something Necessary". Katika filamu hiyo wamemtumia character mmoja mwanamke aitwae Anne ambae anaonesha maisha yake yalivyokuwa baada ya machafuko yaliyoivuruga nchi hiyo mwaka 2007, Anne ni mwanamke anaehangaika kuyarudisha maisha yake aliyokuwa nayo kabla ya machafuko hayo, akijaribu kupambana kwa ajili ya afya ya mtoto wake wa kiume, alipompoteza mumewe, na shamba lake. Lakini pia yumo character mwenye jina la Joseph, yeye ni gang member aliyehusika katika machafuko hayo, lakini wote Joseph na Anne wanajikuta wakiwa katika wakati mgumu wakitafuta jinsi ya kuzifuta kumbukumbu hizo mbaya na kuendelea na maisha yao ya kawaida. Iangalie trailer yake hapa, "Something Necessary"..

No comments:

Post a Comment