Baadhi ya askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakimshusha mwenzao
baada ya kujigonga kwenye mti na kujeruhiwa vibaya na kupasuka sehemu za
kichwani wakati akiwa kwenye Lori lenye namba za usajili 5514 JW 07
aina ya IVECO kandokando ya barabara ya Samora jirani na Idara ya Habari
(Maelezo) jijini Dar es Salaam jioni hii.
Baadhi ya wasamalia wema wakimpeleka hospitali majeruhi huyo.
Majeruhi akiingizwa katika Bajaji tayari kwa ajili ya kupelekwa hospitali.
Lori aina ya IVECO ambalo majeruhi huyo alikuwa amepanda huku likiwa limesheheni mzigo mkubwa.
Majeruhi akipakizwa kwenye bajaj ili kupelekwa hospitalini
Hii ndio Barabara ya Samora ilipotokea ajali hiyo.
Hapa ndipo alipojigonga majeruhi na kupasuka sehemu za kichwani
No comments:
Post a Comment