KONDAKTA
mmoja anayefanyakazi kazi zake katika basi lifanyalo safari zake Tabata
Kimanga Mnazimmoja amejikuta akuuanza mwaka vibaya kwa kujeruhiwa na
abiria baada ya kumdai nauli bibi mzee.
Konda huyo amekutwa na mkasa huo majira ya 2 asubuhi leo akiwa katika kazi yake hiyo ya ukusanyaji hela kwa abiria wake
Wakati akiendelea na zoezi lake hilo katika moja ya siti zilizopo katika basi hilo ilikaliwa na bibi mmoja mzee anayedadiriwa kuwa na miaka zaidi ya 70
Hivyo konda huyo alimtaka bibi huyo ampe nauli yake ili aendelee kukusanya kwa wengine na konda huyo hakufurahiwa na jibu alilotoa bibi huyo kuwa amsamehe kwani hakuwa nayo ndipo alipoamsha mzuka wa konda huyo na kumtaka afungue nauli anakusanya kwa wengine kisha atamrudia
Konda huyo alimaliza zoezi la kukusanya kwa wengine ndipo alipomrudia bibi huyo kumtaka afungue nauli yake la sivyo angemshusha hapo ndipo aliwachokoza baadhi ya abiria waliyokuwemo katika basi hilo
Baadhi ya abiria walimntaka kodna huyo amsamehe bibi huyo kuliongana na umri wake na uzee alionao konda huyo hakutaka kusikia la muazini wala la mnadi swala na kuendlea na msimamo wake wa kutaka nauli
"Naomba nauli yangu, ulitokaje nyumbani kwako bila ya kuwa na nauli, nyinyi ndio wanga mnaotaka kuroga watoto wa wenzenu kwa kuwatafutia sababu"
Kauli hiyo haikupendezwa na wengi ndipo wenye hasira kali walimtaka konda huyo apunguze jazba, alipoonekana anaendelea kumporomoshea maneno bibi huyo alitokea kijana mmoja alitaka amlipie nauli lakini walitokea baadhi ya abiria walisema hakuna kumpa hela huyu bibi atakwenda bure hadi mwisho wa safari yake
Hapo ndipo varangati lilianza rasmi konda huyo alimuamrisha bibi huyo ashuke ndipo akatokea mwanaume mmoja akamuwasha kibao konda huyo, konda akakabidhi pesa kwa dereva na kuanza kurudisha mahsambulizi hali iliyofanya kijana huyo awajibishwe na kujikuta akipatwa na majeraha katika baadhi ya maeneno yake ya usoni huku abiria wakitaka gari likifika eneo la buguruni basi hilo lipelekwe polisi lakini dereva alipitisha hakusimama
Nifahamishe ilishuhudia sakata hilo na alipozungumza na baadhi ya abiria wengine walimlaumu konda huku wengine wakiwashushia lawama abiria wenzao kwa kumjeruhi konda, kwani konda alikuwa na haki ya msingi kudai pesa kwani alikuwa kazini
Mmoja wa abiria aliiambia nifahamishe kuwa, imezoeleka kila Ijumaa mabibi na mababu wanakwenda mjini kuombaomba na yeye alikuwa upande wa kondakta kumdai pesa bibi huyo na kusema wakiwa wanadaiwa nauli wimbi la ombaomba kwenda kuomba mjini litapungua

No comments:
Post a Comment