Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakusudia
kuwatumia wataalamu wa Kitanzania walioko ndani ya nchi na wale walioko
ughaibuni (Diaspora) katika kutekeleza mipango yake kadhaa yenye
umuhimu kwa Taifa.
Hapo
awali, Serikali iliwatumia zaidi wataalamu kutoka nchi nyingine, ambapo
kwa sasa lengo ni kuona kwamba wataalamu wa nchi nyingine wanatumika
pale tu ambapo wataalamu wa Kitanzania walio ndani na nje ya nchi
hawajapatikana kufanya kazi husika.
Katika kutekeleza azma hiyo, Serikali itapenda kupata wataalamu wa Kitanzania kwenye maeneo yafuatayo:-
i)Mfumo mzima wa utafutaji, uchimbaji, uongezaji thamani na usambazaji wa gesi asilia na mafuta.
(ii) Kuimarisha matumizi salama ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kuboresha utendaji wa Serikali na utoaji wa huduma kwa wananchi.
(iii)Kuboresha utekelezaji wa malengo ya Serikali na kupima matokeo kupitia mfumo unaokusudiwa kuhakikisha tunapata matokeo makubwa na ya haraka katika maeneo ya kipaumbele na kimkakati katika maendeleo ya Taifa.

Wataalamu
watakaojitokeza na kukubaliwa kufanya kazi Serikalini katika maeneo
haya, watafanya kazi kwa mikataba ya muda mfupi, lakini inayoweza
kuongezwa iwapo utendaji utaridhisha.
Mwito
unatolewa kwa Wataalamu wa Kitanzania popote walipo,ughaibuni au ndani
ya nchi, kujitokeza na kuleta wasifu wao (CV’s)pamoja na maelezo ya kwa
nini wanafikiri wao ni aina ya watu tunaowatafuta.
Tumia anuani ifuatayo:-
Tumia anuani ifuatayo:-
Katibu Mkuu
Kiongozi
Kiongozi
Ofisi ya Rais, Ikulu
S.L.P. 9120
DAR ES SALAAM.
E.mail:chief@ikulu.go.tz

No comments:
Post a Comment