skip to main |
skip to sidebar
RAIS WA SERIKALI YA WANAFUNZI WA KITIVO CHA SAYANSI YA JAMII- UDOM ATIWA MBARONI KWA WIZI WA MILIONI 15.6
RAISI
WA KITIVO CHA SAYANSI YA JAMII,SANAA NA LUGHA CHA CHUO KIKUU CHA
DODOMA(UDOM) IDD MOHAMED NA WAZIRI WAKE WA FEDHA IBRAHIM MATATA
WASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA WIZI WA SHILINGI MILIONI 15 NA LAKI
6,MALI YA SERIKALI YA WANAFUNZI WA KITIVO CHA SAYANSI YA JAMII,SANAA NA
LUGHA CHA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM)
TAARIFA TOKA KWA MDAU
JOSEPHAT LUKAZA WA LUKAZA BLOG ZINASEMA KUWA RAISI WA KITIVO CHA
SAYANSI YA JAMII, SANAA NA LUGHA AMBAYE PIA NI MWANAFUNZI WA MWAKA WA
TATU ANAYESOMA BCOM ACCOUNTINGANAYEFAHAMIKA KWA JINA LA IDD MOHAMED
ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KITUO CHA POLISI UDOM KWA TUHUMA ZA WIZI
WA FEDHA KIASI CHA SHILINGI MILIONI 15 NA LAKI 6.
MTUHUMIWA HUYO ALIKAMATWA JANA SIKU
YA ALHAMISI AKIWA NA MWENZAKE AMBAYE PIA ALIKUWA WAZIRI WA FEDHA WA
KITIVO HIKO IBRAHIM MATATA AMBAYE PIA NI MWANAFUNZI WA MWAKA WA TATU
BCOM ACCOUNTING NA KUFIKISHWA KATIKA KITUO HIKO CHA POLISI.
MARA
BAADA YA KUKAMATWA WALIKUTWA NA KIASI CHA SHILINGI MILIONI 7 LAKI 2 NA
24 ELFU.(Shilingi 7,224,000 ZA Kitanzania.) Na fedha hizo zilitolewa
kwenye account ya serikali ya wanafunzi kitivo cha Sayansi ya Jamii,
Sanaa na Lugha na kupelekwa katika Akaunti ya Mtu Binafsi ambaye ni
Waziri wa Fedha wa Kitivo hiko Ndugu Ibrahim Matata.
Chanzo hicho kiliendelea
Kujuza kuwa Awali Raisi Huyo Anahusika na kosa la kuomba Rushwa ya
Shilingi Milioni 1 na laki 1 katika Duka lililopo Katika Bweni namba 13
(Block 13 ).
Raisi huyo pamoja na Waziri wake wa Fedha
walikamatwa Jana na kulala katika Kituo Cha Polisi Cha UDOM tayari kwa
Uchunguzi na hatua za kisheria Kuchukuliwa ili kuweza Kufikishwa
mahakamani
Habari zaidi ambazo Lukaza imezipata kutoka katika
Vyanzo vya habari Zinadai kuwa Raisi huyo pamoja na Waziri wake Wa
fedha watafikishwa Mahakamani Jumatatu kwa tuhuma za wizi wa Shilingi
Milioni 15 na laki 6 ambapo waliweza kuzitoa na kuweka katika akaunti ya
Waziri Wa Fedha Ibrahim Matata na kufanikiwa kuchukua Sh Milioni 7 laki
2 na Ishirini na Nne elfu ambazo ndio walikamatwa nazo Mkononi.
Hatimaye
Bunge la Serikali ya Wanafunzi Wa Kitivo Cha Sayansi ya Jamii ,Sanaa na
Lugha Cha Chuo Kikuu Cha Dodoma linatarajiwa kukaa leo Saa 10 Jioni ili
kuweza kutoa uamuzi wa Kumvua madaraka na kufikisha baadhi ya Ushaidi
wa Sauti wakati Raisi huyo akiomba Rushwa katika Duka lililopo Block 13.
No comments:
Post a Comment