Spika
Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania na Waziri wa Afrika
Mashariki Mhe. Samwel Sitta akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya kwa
Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano baina yao katika
ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo (jumatatu januari 21, 2013).
Kushoto ni Mjumbe wa Tume Bi. Maria Kashonda.
Spika
Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Afrika
Mashariki Mhe. Samwel Sitta (katikati) akiagana na Wajumbe wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi (kushoto) na Bw. Nassoro
Mohammed (kulia) mara baada kiongozi huyo kuwasilisha maoni yake kuhusu
Katiba Mpya katika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi
wa Mashtaka Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi akitoa maoni kuhusu Katiba Mpya
katika mkutano kati ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Tume ya
Mabadiliko ya Katiba leo (jumatatu januari 21, 2013) jijini Dar es
Salaam. Kushoto kwake ni Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George
Masaju na Wajumbe wa Tume Bw. Humphery Polepole na Bw. Awadhi Said.
Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Mohammed Hamad akitoa ufafanuzi kuhusu majukumu ya kitengo cha utafiti cha Tume kwa ujumbe wa Tume ya Kurekebisha Sheria (LRCT) ulioongozwa na Makamishina wa Tume hiyo, Jaji Ernest Mwipopo (wa tatu kulia) na Bi. Esther Manyesha (wa nne kulia). LRCT imewasilisha maoni kuhusu Katiba Mpya kwa Tume leo
Kamishina
wa Tume ya Kurekebisha Sheria (LRCT) Jaji Ernest Mwipopo akikabidhi
maoni ya LRCT hiyo kuhusu Katiba Mpya kwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko
ya Katiba, Prof. Mwesiga Baregu katika ofisi za Tume jijini Dar es
Salaam leo (jumatatu januari 21, 2013). Katikani ni Mjumbe wa Tume Bw.
Simai Mohammed.
Mjumbe wa
Mtandao wa Kinga Jamii (TPSN - Tanzania Social Protection Network) Bi.
Clotilda Isdor akitoa maoni kuhusu Katiba Mpya katika mkutano na wajumbe
wa Tume ya Mabadiliko uliofanyika leo (jumatatu janauari, 21, 2013). Wa
kwanza kushoto ni Mjumbe wa Tume, Bi. Mwatumu Malale.
No comments:
Post a Comment