Wahandisi
wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakikamilisha kufunga kioo kipya
ambacho kimenunuliwa kutoka nchini Marekani cha ndege yao aina ya
Dash-8 Q300 yenye namba za usajili SH-MWF ambayo ilipata ufa (Wind
Shield Crack) tarehe 11 Januari, 2013, muda mfupi baada ya ndege hiyo
kuruka kutoka Kigoma kurudi Dar Es Salaam katika safari zake za kawaida.
Matengenezo
hayo yanafayika katika uwanja wa ndege wa Kigoma yakisimamiwa na
Mhandisi Righton Mwakipesile na Mhandisi Merkior Karwani
Uongozi
wa ATCL umedhibitisha kuwa safari za Dar-Kigoma-Dar zitaendelea kama
ratiba yao inavyoonyesha punde kuanzia kesho tarehe 22/1/2013.
No comments:
Post a Comment