Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, February 7, 2013

FAST JET YAKANUSHA TAARIFA KWAMBA WAMEPOKONYWA LESENI YA KUFANYA BIASHARA SOMA HAPA.

Kampuni ya ndege ya Fast Jet imezikanusha ripoti kuwa imenyang’anywa leseni yake ya biashara katika nchi kadhaa barani Afrika ikiwemo Tanzania.Kupitia website yake kampuni hiyo imeandika

Licha ya taarifa za leo kwenye vyombo vya habari, ni biashara kama kawaida hapa fastjet. Madai kuhusu kunyang’anywa leseni ni uongo mtupu.  Tunaendelea na safari zetu kutoka Tanzania na tunaendelea kuanzisha safari mpya kama ilivyopangwa.

Hii ni njama/hujuma ‘binafsi’ dhidi  ya fstjet katika jaribio wazi lililotengenezwa kuharibu brand na sifa ya Fastjet.Ofisi zetu na matawi yetu bado zipo wazi kwa booking mpya na hakuna refund zozote. Taarifa rasmi itapatikana masaa machache yajayo.

No comments:

Post a Comment