Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama
Salma Kikwete akimshika kwa furaha mtoto aliyezaliwa tarehe 5.7.2013
katika hospitali ya Mkoa wa Lindi, Sokoine huku mama wa mtoto huyo
Muksim Issa ,19, anayetoka katika kijiji cha Mumbu kilichoko katika
wilaya ya Lindi vijijini aliyelala kitandani akitabasamu. Mtoto huyo
alizaliwa akiwa na uzito wa kilo 3.9 Mama Salma alitembelea hospitalini
hapo kukabidhi vifaa vya hospitali tarehe 6.2.2013. Aliyesimama kulia
kwa Mama Salma ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi Dr. Nasoro Hamid.
PICHA NA JOHN LUKUWI
Kikundi
cha utamaduni kikiwatumbuiza waalikwa kwa ngoma ya Tambiko inayochezwa
na watu wa kabila la Wamakonde wakati wa sherehe ya kukabidhi vifaa vya
tiba kwenye hospitali kuu ya mkoa wa Lindi, Sokoine, tarehe 6.2.2013.
Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia viongozi na wafanyakazi wa
hospitali ya mkoa wa Lindi, Sokoine,na wananchi waliohudhuria sherehe ya
kukabidhi rasmi vifaa vya tiba kwenye hospitali hiyo tarehe 6.2.2013
huko Lindi Mjini. Waliokaa kushoto kwa Mama Salma ni Kaimu Mganga
Mfawidhi wa hospitali Dr. Nicolaus Munni, Mwenyekiti wa Bodi ya
Hospitali ambaye pia ni Meya wa Lindi Mjini Ndugu Frank Magali na wa
mwisho ni Mwakilishi wa Project C.U.R.E. nchin Tanzania Bwana Makembe
Kimario.

wa Rais Mama Salma Kikwete akikata utepe kuashiria kukabidhi rasmi kwa
vifaa vya hospitali ya mkoa wa Lindi,Sokoine, vilivyotolewa na Taasisi
ya WAMA kwa kushirikiana na Shirika la Project C.U.R.E. la nchini
Marekani. Vifaa hivyo vina thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia
saba. Kulia kwa Mama Salma ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi ambaye pia ni
Mkuu wa wilaya ya Lindi Dr. Nasoro Hamidi akifuatiwa na Katibu wa CCM WA
Mkoa huo Ndugu Adelina Gefi na kushoto ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa
hospitali Dr. Nicolaus Munni. Sherehe hiyo ilifanyika tarehe 6.2.2013.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA,
Mama Salma Kikwete kwa furaha akiagana na wafanyakazi wa hospitali ya
Mkoa wa Lindi,Sokoine, viongozi na wananchi waliohudhuria sharehe za
kukabidhi vifaa vya hospitali hiyo tarehe 6.2.2013.
No comments:
Post a Comment