Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, February 17, 2013

HUYU ndo "SISTER" ALIYEFUMANIWA HATIMAYE AHUKUMIWA.....


MAHAKAMA ya Mwanzo mjini hapa,  imemtia hatiani aliyekuwa mtawa wa Shirika la Kitawa la Kanisa Katoliki Jimbo la
Sumbawanga, Sista Yasinta Sindani, kwa kufumaniwa na mume wa mtu na kuamriwa kumlipa fidia ya Sh 700,000 mlalamikaji. 

Katika kesi ya msingi ya madai, mlalamikaji Asteria Mgabo alimtaka Sista Yasinta amlipe Sh milioni 3 baada ya kumfumania na mumewe wa ndoa, Martin Msangawale (39) ambaye pia ni mkazi wa mjini hapa. 
Sista huyo ambaye ni daktari katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa mjini hapa, kwa sasa anaishi nje ya nyumba ya utawa eneo la Kantalamba.

Katika hati ya awali ya madai, inadaiwa mshitakiwa alifumaniwa na Asteria akiwa na mumewe Msangawale wakiwa kwenye nyumba ya kulala wageni  ijulikanayo kwa jina la Chipa iliyopo eneo la Katandala mjini hapa, Desemba 24  mwaka jana majira ya saa 7 usiku  ikiwa ni siku ya mkesha wa Sikukuu ya Krismas.

Akisoma  hukumu  hiyo juzi, hakimu wa  mahakama  hiyo, Jaffar Mkinga alisema kuwa ushahidi uliotolewa na mlalamikaji ulikuwa mzito wenye kuondoa shaka zote  kuwa mdaiwa alitenda kosa hilo tofauti na utetezi  uliotolewa na mdai kuwa ulikuwa dhaifu.

Awali katika  utetezi wake  mdaiwa  aliiambia mahakama  hiyo kuwa  kwanza alikuwa hajui kuwa Martin alikuwa  mume wa mtu na kukiri mbele ya mahakama hiyo kuwa alimweleza kuwa hana mke hivyo alimwomba amuoe. 

Lakini Hakimu Mkinga alipinga utetezi huo kwa sababu usiku  huo wa mkesha  wa Krismas  mwaka jana, saa saba na robo usiku, mlalamikaji akiongozana na mwenyekiti wa mtaa wakiwa na mashahidi wengine watatu,  walimkuta mdaiwa na Martin wakitoka katika   moja ya vyumba katika nyumba ya kulala  wageni ya Chipa, akasainishwa. 

“Kama hukufahamu kuwa Martin alikuwa  hana  mke ilikuwaje ukakubali kusaini karatasi hiyo ya fumanizi  iliyoandaliwa na mwenyekiti  huyo?” alihoji hakimu, akamhukumu kulipa sh 700,000.

No comments:

Post a Comment