Mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA kupitia kitengo cha maudhui imevifungia matangazo kwa muda wa miezi sita vituo vya radio viwili nchini kwa kukiuka maadili ya utangazaji.
Vituo hivyo ni pamoja na Kwa Neema FM ya Mwanza iliyofungiwa kwa kuendesha mjadala uliokuwa ukihusiana na watu wa dini gani wenye haki ya kuchinja wanyama kati ya waislam na wakristu hali iliyosababisha mgongano wa waumini wa dini hizo.
Kingine ni Imani Radio FM ya mjini Morogoro ambayo imefungiwa kwa kosa la kupinga zoezi la sensa mwaka jana na kuwashawishi waumini wa dini ya kiislam wasijiandikishe.
Nayo Clouds FM imepigwa faini kwa kuendesha mjadala kuhusiana na ushoga pamoja na kuwa na kipengele kwenye kipindi cha Power Breakfast kiitwacho ‘Jicho la Ng’ombe’ ambacho wametakiwa wakifute kutokana na kuendeshwa kinyume na maadili.
No comments:
Post a Comment