Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, February 26, 2013

HAYA NDO MANENO ALIYOANDIKA DJ CHOKA KWENYE UKURASA WAKE WA FACEBOOK KUHUSIANA NA MATANGAZO YANAYOWEKWA KWENYE BLOGS.

 
NGOJA NISEME YAMOYONI:
Leo ningependa kuongea na hawa makampuni makubwa wanaopenda kutangaza kupitia BLOG'S mbalimbali hapa nchini. Sipendi kuyataja majina ila nitajisemea mimi mwenyewe yanavyonikera sitosemea blog's za wenzangu, hivi kwanini nyie makampuni makubwa makubwa mnaringa sana inapofika muda wakutoa hela zakutulipa sisi watu wachini ukiachilia mbali hao wajuu kama TV & Radio mnaowahi kuwapa hela zao bila usumbufu? mjibu basi mtu hela itatoka siku fulani au tarehe fulani, sasa wewe unapigiwa simu hupokei ukipokea unasema bado bado sikilizia, hiyo sikilizia inakwenda hadi miezi mitatu halafu mimi ndio hela ninayoitegemea kuendesha maisha yangu na familia yangu.

Kuna wenzangu na mie wataweza kuvumilia coz wengine wako maofisini so mshahara utatoka utawasukuma kidogo haya mie ninayekesha usiku kutafuta matukio narudi saa kumi na mbili asubuhi, hapo hapo nikiamka kazi yangu nikuwasha laptop nakuzima nakuzurura kutafuta matukio huyo mwenzangu yupo ofisini anasubiri COPY & PASTE maisha yaendelee basi tu anajulikana na nyie wakubwa huko ofisini ndio mtampa hela haraka.

INAKERA SANA HESHIMUNI KAZI ZA MIKONO YA WATU HASWA PALE MNAPOKIONA NI KIZURI BASI MPENI NGUVU ILI AENDELEZE UZURI HUO NA SIO KUMDIDIMIZA NA KUISHIA KUKOPA MKIJA KUMLIPA HELA YOTE INAISHIA DUKANI KWA MANGI NA SEHEMU ZINGINE ALIZOKOPA. Kama kuna mtu nimemkera kwa kuongea haya yangu ya moyoni naomba SAMAHANI. Nimemaliza

DJ CHOKA

No comments:

Post a Comment