Picha hii si ya tukio hilo...
OPERESHENI
ya kuwasaka wezi wa maji Dar es Salaam, juzi imechukua sura mpya baada
ya mkazi wa Tandale Chama, wilayani Kinondoni ambaye ni mwanamke , kuvua
nguo zote.
Chanzo cha mwanamke huyo kuvua nguo ni baada ya kuuona msafara wa Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Meck Sadiki na Maofisa
wa Shirika la Maji Safi na Maji Taka (DAWASCO), ambao walimkuta akiuza maji aliyojiunganishia kiholela.
Hata
hivyo, Ofisa wa DAWASCO ambaye ni mwanamke alilazimika kumkamata na
kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi waliokuwa katika operesheni hiyo.
Operesheni
hiyo ilifanyika kwenye eneo la Kagera, Tandale Chama, Mkwajuni na Bonde
la Mkwajuni ambapo vifaa mbalimbali ambavyo vilikuwa vikitumika
kuunganisha maji vilikamatwa.
Mkuu
wa Mkoa huo, Bw. Sadiki alisema operesheni hiyo imefichua mambo mengi
yanayofanywa na wananchi aliowaita wahujumu uchumi kwa kujiunganishia
maji kiholela bila kuyalipia.
Alisema asilimia 36 ya maji yamekuwa yakipotea kutokana na baadhi ya watu kujiunganishia kichume cha sheria.
No comments:
Post a Comment