Rais mpya wa Korea Kusini Park Gun-Hyeh (pichani) ameapishwa katika sherehe zilizofanyika kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Seoul.
Watu elfu 70 wamehudhuria sherehe hizo zilizofanyika kwenye jengo la bunge la nchi hiyo.
 Akihutubia baada ya kuapishwa, Mwanamama Park ameitolea wito Korea Kaskazini kuachana na mpango wake wa nyuklia na kuacha kutumia vibaya rasilimali katika kutengeneza silaha.
Bibi Park ni mwanamke wa kwanza kuwa rais nchini Korea Kusini na ni mtoto wa kiongozi na mwanajeshi wa zamani wa nchi hiyo hayati Park Chung-Hee.