Kiongozi wa Cuba Raul Castro amechaguliwa tena kuwa rais wa nchi hiyo na ametangaza kwamba ataondoka madarakani baada ya kipindi chake kukamilika mwaka 2018.
Raul Castro mwenye umri wa miaka 81 alichukua rasmi madaraka ya urais mwaka 2008, miaka miwili baada ya kuchukua nafasi ya kaka yake Fidel Castro.
Bunge la Kikomunisti la Cuba limemchagua pia Miguel Diaz-Canel Bermudez kuwa Makamu wa kwanza wa rais.
Diaz-Canel mwenye umri wa miaka 52 anaonekana kuwa mrithi wa Castro.